Kijue alichokifanya serena william baada ya kumshinda mpinzani wake christina hchale.soma zaid.
Nyota wa mchezo wa tenisi kwa upande wa
wanawake Serena Williams alijitia ugonjwa
baada ya kula chakula cha mbwa saa chache
kabla ya kufuzu katika robo fainali ya
mashindano ya Italian Open.
Serena alijaribu kula kijiko kimoja cha chakula
cha mbwa wake kabla ya kumshinda Mmarekani
mwenzake Christina McHale katika seti za moja
kwa moja.
''Nilisema kwani kuna nini,nitajaribu kipande
kimoja,kinaonja utamu'',alisema.
''Lakini mda mchache nililazimika kukimbia
chooni kama ambaye ningezimia''.
''Chakula kilikuwa na ladha mbaya''.
''Kinaonja kama dawa ya kusafisha
nyumba''.Katika video ya Snap chat ,wiliams
alielezea kuwa alichukua samaki na wali uliokuwa
katika chakula kilichopewa mbwa katika hoteli
aliyokuwa akilala.
''Nilijilazimisha kula'',alisema mchezaji huyo wa
Marekani mwenye umri wa miaka 34.
''Sijui wanatia nini katika chakula hiki cha
mbwa,lakini mbwa alikipenda sana''.chanzo bbc
0 comments :
Post a Comment