Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 19, 2016

Mhandisi wa wilaya ya Bunda asimamishwa kazi.soma zaid.

Serikali mkoani Mara imemsimamisha kazi
mhandisi wa umwagiliaji wilaya ya Bunda Bw
Nuni Munyobelege kwa madai ya kuendesha
hujuma na kushindwa kutatua mgogoro kati ya
pande mbili zinazovutana katika skimu ya
umwagiliji ya kisangwa hatua ambayo
imesababisha mradi huo mkubwa kushindwa
kufanya kazi kwa muda mrefu sasa licha ya
serikali kutumia zaidi ya shilingi bilioni moja na
milioni mia nne kwa ujenzi wa mradi huo.
Mkuu wa mkoa wa Mara Bw Magesa Mulongo,
amechukua hatua hiyo ikiwemo na kuifuta kamati
yote inayosimamia mradi huo, baada ya
kutembelea na kupata maelezo juu ya utekelezaji
wa mradi huo wa mwaka 2007 na kubaini kuwa
pamoja na serikali kutoa kiasi hicho kikubwa cha
fedha ili kuwezesha wananchi wa vijiji vya kata
ya mcharo kutumia skimu hiyo kwa kilimo cha
umwagiliaji, lakini idara ya umwagiliji imeshindwa
kutatua mgogoro katika eneo hilo na kusababisha
mradi huo kukwama.
Nao baadhi ya viongozi wa halmashauri ya mji
wa Bunda, wameunga mkono hatua ambazo
zimechukuliwa na mkuu wa mkoa wa Mara, huku
wakitoa ahadi ya kufanya uchunguzi wa kina
kuhusu kwakwama kwa mradi huo, kisha
kuchukua hatua kali kwa wahusika.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa wa
Mara amemvua uenyekiti wa serikali ya kijiji cha
Nyarigamba “A” Bw Sitta Masalu na kuagiza
kukamatwa na jeshi la polisi baada kudaiwa
kumpiga kichwa hadharani mwananchi mmoja wa
kijiji hicho na kumsababishia majeraha makubwa
kichwani.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top