Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 19, 2016

Walimu wametawanya kwa mabomu wilawani Bukombe mkoani Geita. soma zaid.

Jeshi la Polisi wilayani Bukombe mkoani Geita
lalazimika kutumia mabomu ya machozi
kuwatawanya walimu waliokuwa wamefika
kwenye ofisi za mkurugenzi wa halmashauri hiyo
kwa lengo la kumweleza matatizo
yanayowakabili.
Hatua hiyo imekuja baada ya walimu hao pamoja
na viongozi wa chama cha walimu wilaya ya
Bukombe kuzuiliwa na askali polisi kutoingia
kwenye lango kuu la ofisi za mkurugenzi kwa
madai kuwa hawajatoa taarifa ya kufanya
maandamano wala mkusanyiko usio halali.
Baada ya kuzuiliwa kuingia katika ofisi hizo za
halmashauri ya wilaya ya Bukombe walimu
walianza kuimba na kulilazimu jeshi la polisi
kufyatua mabomu.
Walimu hao wanamadai 17 yakiwemo mishahara
ya walimu wanaodai tangu mwaka 2010 ambayo
ni zaidi ya sh, 150 milion, mapunjo ya mishahara
ambayo ni zaidi ya milion 259.
Like

0 comments :

Post a Comment

Back To Top