Mifuko ya sukar 1060 yakamatwa mkoani mwanza na polisi.
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana
na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani
humo limekamata kontena lenye mifuko 1060 ya
Sukari sawa na tani 26.5 mali ya Adam Balenga
ambayo inadaiwa kununuliwa kutoka kwenye
kampuni ya Al–Neem Enterprises ya jijini Dar es
Salaam, baada ya nyaraka za ununuzi wa Sukari
hiyo kuonekana kuwa na utata.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza kamishna
msaidizi mwandamizi Ahmed Msangi amesema
shehena hiyo ya Sukari hiyo, yenye thamani ya
shilingi milioni 53 imekamatwa mei saba mwaka
huu majira ya saa kumi jioni katika mtaa wa rufiji
jijini Mwanza, ikiwa ndani ya gari lenye namba za
usajili T.200 BSV lori aina ya Scania na tela lake
lenye namba T.601 DFM wakati likifaulisha Sukari
hiyo kwenye magari mengine madogo manne na
kwenye bajaji mbili.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella
ameongoza wajumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa huo kushuhudia kontena hilo la
Sukari linaloshikiliwa katika kituo kikuu cha polisi
cha wilaya ya Nyamagana.
Wakazi wa jiji la Mwanza pia wanalia na uhaba
wa Sukari ambao umesababisha kilo moja
kuuzwa kwa bei ya kati ya shilingi 4500 hadi
5000 tena kwa kificho.
Mohamed Sharif ni mfanyabiashara wa Sukari
jijini Mwanza anaeleza nini kifanyike kukabiliana
na hali ya uhaba wa Sukari unaosababishwa na
baadhi ya wafanyabiashara kuficha Sukari.
0 comments :
Post a Comment