Mkuu wa mkoa aagiza kukamatwa kwa mkurugenzi mtendaji na muweka hazima na wafikishwe mahakamani.soma zaid.
MKUU wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo
ameagiza polisi mkoani humo kuwakamata na
kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria aliyekuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Simon
Mayeye na aliyekuwa Mweka Hazina, Emmanuel
Joramu ili waweze kuhojiwa kuhusu ubadhirifu
wa mamilioni ya fedha za serikali.
Mulongo ametoa agizo hilo juzi kwenye kikao cha
majumuhisho ya ziara yake aliyoifanya wilayani
Bunda na kuagiza kuwa watuhumiwa wote
wakabidhiwe kwa Taasisi ya Kupambana na
Kuzuia Rushwa (Takukuru) pamoja na Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG).
Agizo hilo alilitoa kutokana na taarifa ya baraza
la madiwani iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Issack Mayela
inayohusu ubadhirifu huo wa mamilioni ya fedha
ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 2.3, zikiwemo za
ulipaji fidia wananchi wa kijiji cha Tairo ili
kupisha eneo la uwekezaji (EPZ).
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa watumishi
hao wa serikali ambao kwa sasa wamehamishiwa
katika halmashauri nyingine watafutwe popote
pale walipo na wakamatwe mara moja na
kuhojiwa na kisha kutoa maelezo yao polisi, ikiwa
ni pamoja na hatua za kinidhamu na za kisheria
kuchukuliwa dhidi yao.
“Huyo Mkurugenzi na Mweka Hazina ambao
wametajwa katika taarifa hizo watafutwe mahali
popote walipo na kisha kuhojiwa dhidi ya
ubadhirifu huo na hatua za kinidhamu na kisheria
zichukuliwe dhidi yao…kazi hii naikabidhi CAG na
Takukuru na waikamilishe ndani ya siku 14,”
alisema.
0 comments :
Post a Comment