Breaking News
Loading...

Advert

Friday, May 20, 2016

Wizara yafuta leseni 1,330 za utafutaji na uchimbaji madinii.soma zaid.

LESENI 1,330 za utafutaji madini na uchimbaji
mdogo wa madini zimefutwa na Wizara ya
Nishati na Madini kati ya Julai, 2015 na Machi,
2016.
Aidha, maombi 2,716 ya leseni yalikataliwa kwa
kushindwa kukidhi masharti.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo, kati ya hizo, leseni
151 zilikuwa ni za utafutaji madini na 1,179 ni za
uchimbaji mdogo wa madini.
Akiwasilisha bajeti yake ya mwaka 2016/17
bungeni, Profesa Muhongo alisema hati za
makosa 117 zilitolewa kwa leseni 111 za
utafutaji madini na sita za uchimbaji wa kati.
“Napenda kutoa mwito kwa wamiliki wa leseni za
madini kutimiza masharti yaliyowekwa kwenye
leseni hizo ili kuepuka kuchukuliwa hatua za
kisheria ikiwemo kufuta leseni hizo,” alisema.
Aidha alisema hadi kufikia Machi, 2016 jumla ya
leseni 4,803 za utafutaji na uchimbaji madini
zilisajiliwa kwenye Mfumo wa Kupokea Maombi
ya Leseni kwa Njia ya Mtandao (OMCTP), kati ya
leseni 38,695 zilizopo.
Alisema kati ya leseni hizo zilizosajiliwa, leseni
1,628 ni za utafutaji mkubwa wa madini, leseni
65 ni za uchimbaji mkubwa na wa kati na leseni
3,110 ni za uchimbaji mdogo.
“Kwa upande wa umiliki wa leseni za utafutaji na
uchimbaji mkubwa wa leseni zote, Watanzania
wanamiliki asilimia 68 ya leseni zote, wageni
asilimia 28 na asilimia nne zinamilikiwa kwa ubia
kati ya Watanzania na wageni… leseni za
uchimbaji mdogo ambazo ni 35,273 zinamilikiwa
kwa asilimia 100 na Watanzania,” alieleza.
Aliongeza kuwa kati ya Julai 2015 na Machi 2016
jumla ya maombi ya leseni 8,025 ya utafutaji na
uchimbaji madini yalipokelewa na kwamba jumla
ya leseni 4,782 zilitolewa, ambazo kati ya
hizo,112 ni za uchimbaji mkubwa wa madini,
leseni 12 za uchimbaji wa kati, lesenimoja ya
uchimbaji mkubwa na leseni 4,657 ni za
uchimbaji mdogo wa madini.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top