Breaking News
Loading...

Advert

Friday, May 6, 2016

Serikali inusuru migogoro ya wafugaji na wakulima wilayabi mvomero.soma zaid.

Licha ya serikali kuanza kuweka mpaka wa
mfereji mkubwa wa kutenganisha eneo la
wafugaji wa kijiji cha Kambala na wakulima wa
bonde la Mgongola lakini bado uvunjifu wa amani
umeendelea kujitokeza baada ya wafugaji
kuamua kuvuka mpaka huo na kuvamia na
kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima.
Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya
Mvomero Betty Mkwasa wakulima hao
wamesema wanasikitishwa na kitendo cha
wafugaji hao kuvuka mpaka uliwekwa na serikali
na chini ya uamuzi wa mahakama ambapo
wamemuomba Raisi John Magufuli kupeleka
wanajeshi ambao watasaidia kutatua kero hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Betty Mkwasa
amelazimika kutumia usafiri watrekta kwenda
kujionea hali ilivyo kati ya wakulima na wafugaji
mashambani nakushughudia vitendo vya uvunjifu
wa amani baada ya ng’ombe kuingia katika
mashamba ya wakulima ambapo amewataka
wakulima kufuata sheria huku akiagiza kuundwa
vikundi vya ulinzi na usalama kwa wakulima na
wafugaji vitakavyo tambuliwa na serikali
ilikusaidia ulinzi katika makundi hayo mawili.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top