Breaking News
Loading...

Advert

Friday, May 6, 2016

Wafanyabiashara wadogowadogo watagawiwa mashine ya EFD's jumla 5,700 bure

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Alphayo Kidata
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa
makusanyo ya mapato nchini kulia ni
Kamishna wa kodi za ndani
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imejipanga kugawa jumla ya mashine
5700 za (Electronic Fiscal Devices) EFD’s
kwa wafanyabiashara wadogo wadogo
nchini ikiwa ni jitihada za Serikali katika
kukusanya mapato nchini.Akizungumzia
mipango hiyo leo, Jijini Dar es Salaam,
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema
wameamua kuanza kugawa mashine hizo
kwa wafanyabiashara wadogowadogo
ambao wengi wao hawana uwezo wa
kugharamia manunuzi ya mashine hizo.
“ Mamlaka imeona changamoto
wanayoipata wafanyabiashara wadogo
hivyo imeamua kuanza kugawa mashine
hizi ili kuondokana na tatizo la kutotoa
risiti za mauzo kwa wafanyabiashara hao
ambao walio wengi walikuwa na
kisingizio cha kutokuwa na mashine
hizo”. Alisema Kidata.
Kamishna Kidata ameongeza kuwa
Mamlaka yake imeshaagiza mashine hizo
na zipo tayari kuanza kugawiwa mwezi
huu kwa wafanyabiashara hao ikiwa ni
awamu ya kwanza ya ugawagaji wa
mashine hizo ambao utafanyika nchi
nzima.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imeazimia kugawa mashine laki mbili kwa
wafanyabiashara wadogo wadogo nchini
ikiwa ni jitihada za kuweza kukusanya
mapato yatokanayo na kodi za biashara
kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top