Taifa linapateza nguvu kazi ya vijana kutoka na matumizi ya madawa ya kulevya.soma zaid.
Serikali imefanikiwa kukamata takribani
kilo 139.69 za dawa za kulevya ikiwemo
kilo 53.49 za Heroin, Cocaine kilo 86.2
kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka
huu.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya
habari kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti
wa Dawa za Kulevya iliyotolewa na Mkuu
wa Kitengo cha Elimu, Habari na Takwimu
wa tume hiyo, Amani Msami, pia tume
hiyo imekamata tani 97 za bangi na
mirungi.
Alisema mbali na kukamata kilo hizo,
takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa
Heroin nchini wanakadiriwa kuwa kati ya
200,000 hadi 425,000 ambapo kati ya
hao 30,000 hutumia dawa hizo kwa njia
ya kujidunga sindano.
“Serikali imefanikiwa kukamata takribani
kilo 53.49 Heroin, Cocaine kilo 86.2
kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka
huu” alisema Msami na kuongeza kuwa:
“Watumiaji wa Heroin nchini wanakadiriwa
kuwa kati ya 200,000 hadi 425,000
ambapo kati ya hao 30,000 hutumia dawa
hiyo kwa njia ya kujidunga”.Msami
alifafanua kuwa mbali na kukamata dawa
hizo, tume hiyo ilikamata tani 81.3 za
bangi na Mirungi tani 15.7.
Aliongeza kuwa mbali na hayo idadi ya
watuhumiwa waliyokamatwa wakijihusisha
na usafirishaji wa dawa za kulevya
zikiwemo Bangi,Mirungi, Heroin na
Cocaine walikuwa 14,503.Hata hivyo,
alisema takwimu hizo zinaonyesha jitihada
za serikali katika kukabiliana na biashara
ya dawa za kulevya nchini na si ukubwa
wa usafirishaji wa Heroin na Cocaine
nchini.
“Moja ya jitihada za Serikali katika
kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya
ni kutungwa kwa Sheria ya kudhibiti na
kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya
mwaka 2015.” Alisema Msami.
Alifafanua kuwa sheria hiyo imeweka
adhabu kali kwa makosa ya kujihusisha
na matumizi na biashara ya dawa ya
kulevya ikiwemo kifungo cha maisha kwa
yeyote atakayesafirisha dawa za kulevya.
0 comments :
Post a Comment