Breaking News
Loading...

Advert

Monday, May 23, 2016

Tibaijuka yamkuta tena.soma zaid.


Dodoma. Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa
Anna Tibaijuka na Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk
Charles Mlingwa wamelipuliwa bungeni
wakidaiwa kudaiwa kutumia madaraka yao
vibaya.
Tuhuma hizo zilitolewa jana na wabunge wa
upinzani Conchesta Rwamlaza (Viti Maalum -
Chadema) na Dk Godwin Mollel (Siha - Chadema)
walipokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
Rwamlaza alidai kuwa katika Kijiji cha Kamwila
wilayani Muleba, Profesa Tibaijuka akiwa
serikalini, aliomba eka 1,098 lakini hivi sasa
anamiliki eka 4,000 jambo ambalo linazua
mgogoro na wananchi.
“Hili linaleta matatizo kwa kuwa haiwezekani mtu
awe na eneo hilo lote halafu anakodisha kwa
wananchi,” alisema Rwamlaza.
Alisema kuna haja ya kwenda kupima ardhi hiyo
na kama Profesa Tibaijuka aliomba heka 1,098
apewe hizo na si kumiliki eka 4,000 alizonazo hivi
sasa.
Dk Mollel alimtaka Waziri Mkuu amhamishe Dk
Mlingwa akidai ni tatizo katika wilaya hiyo.
Alisema juzi ulitokea mgogoro kati ya wananchi
wa Arumeru na Siha katika mpaka jambo
lilisababisha kubomoleana nyumba.
“Mkuu wa Wilaya alifika pale akiwa amelewa na
kusababisha wananchi kuchukua hatua hizo
wakati ilitakiwa tu tutumie akili,” alisema Dk
Mollel.
Dk Mollel alisema kama DC huyo ataendelea
kuwa na tabia hiyo, migogoro haitaisha na
wawekezaji hawatawaheshimu wananchi kwa
kuwa kiongozi wao anawaaibisha.
“Kama hamtamtoa huyu DC ambaye anatuaibisha
kwa kuomba vitu vidogovidogo kwa wawekezaji
basi sisi tutamtoa kwa kuwa hatuhitaji aibu.”
Alisema kuna haja ya kwenda kupima ardhi hiyo
na kama Profesa Tibaijuka aliomba eka 1,098
apewe hizo na si kumiliki eka 4,000 alizo nazo
hivi sasa.
Dk Mlingwa ajibu tuhuma
Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Mlingwa alisema
tangu kipindi cha kampeni, mbunge huyo alikuwa
akimshambulia kwa maneno ya uongo ili kupata
kura za huruma.
“Hata hii leo (jana) asubuhi alinitumia meseji
akisema ooh nakwenda kukushtaki kwa Rais na
Waziri Mkuu, akaweka na maneno ya vitisho mimi
nikamwambia nenda kwa vile yote ni uongo,”
alisema.
“Nadhani kwa sababu ya ahadi za uongo
alizokuwa nazo kuwa akichaguliwa yeye
mashamba yote ya wawekezaji yaliyoko Siha,
yatakuwa mikononi mwa wananchi jambo ambalo
haliwezekani.”
Dk Mlingwa alisema wawekezaji hao wana hati
za kumiliki mashamba hayo na hilo ndilo ambalo
Serikali imekuwa ikiwaeleza wananchi ukweli ili
kuepuka propaganda za uongo za mbunge.
“Hiyo ndiyo imemfanya aendelee kumsema
vibaya mkuu wa wilaya na mkurugenzi katika kila
nafasi anayoipata hata hayo aliyoyasema bungeni
ameniambia kwa meseji leo atayasema,” alisema.
“Mkuu wa wilaya kwa bahati nzuri hawezi
kujificha tabia na matendo yake kama ningekuwa
mlevi wananchi wangeshasema.”
Wabunge wamvaa Lukuvi
Wabunge wamemshushia ‘zigo’ la migogoro ya
ardhi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi wakimtaka atatue
migogoro hiyo kwa kasi ambayo ameanza nayo.
Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, jana,
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema),
Joshua Nassari alizungumzia mgogoro wa ardhi
katika Wilaya ya Arumeru na kusema mgogoro
huo umekuwapo tangu mwaka 1993.
Nassari alinukuu tangazo katika gazeti la Serikali
na kusema Rais alitangaza kufuta umiliki wa
shamba hilo. Hata hivyo, alisema mwekezaji huyo
aliendelea kumiliki shamba hilo na kuwakataza
wananchi kulima.
“Huyu Mzungu ni nani? Kwa nini anakuwa na
nguvu kuliko Serikali? Rais alitangaza kufuta
umiliki wa shamba hilo tangu mwaka 1993, lakini
mpaka leo anaendelea kumiliki eneo hilo wakati
halitumii,” alisema.
Alisema wananchi wanapodai ardhi yao
wanafunguliwa kesi za kusingiziwa na kufungwa.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Bupe
Mwakanata alimtaka waziri Lukuvi kushughulikia
mgogoro wa shamba la Efatha, uliodumu kwa
muda mrefu bila kutatuliwa.
“Serikali iwasaidie wananchi wake kwa
kuwarudishia ardhi yao ambayo haitumiki
kikamilifu. Wananchi wa eneo hilo wanategemea
kilimo, ukiwanyang’anya ardhi unawasababishia
ugumu wa maisha,” alisema.
Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini
alizungumzia mgogoro katika eneo linalozunguka
Ziwa Chala. Alisema eneo hilo amepewa
mwekezaji ambaye anawazuia wananchi kutumia
maji na kusababisha mgogoro kati ya wananchi
na mwekezaji na kati ya wananchi na Serikali.
“Ziwa Chala ndiyo pekee ambalo asilimia 85 ya
maji yake ni safi na salama na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam wako pale kufanya utafiti.
Tunaomba umalize mgogoro huo, ili wananchi
watumie ziwa hilo na ardhi kwa ajili ya kilimo,”
alisema Selasini.
Mbunge wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso
alisema Mkoa wa Katavi una migogoro mingi
ambayo inasababishwa na mipaka kati ya vijiji
hivyo na Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Alisema vijiji vya Kapanga, Lugonesi, Kabage na
Nkungwi vinakabiliwa na mgogoro ya ardhi
ambayo inawafanya wananchi wa maeneo hayo
kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji.
“Ninaomba wakati waziri anashughulikia
migogoro ya ardhi atuangalie na sisi mikoa ya
pembezoni. Tuna migogoro mingi ambayo
haijapatiwa ufumbuzi na Serikali haijafanya
jitihada zozote,” alisema.
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM),
Omary Mgumba alisema kumekuwa na mgogoro
kati ya Mkoa wa Morogoro na Pwani kwenye vijiji
vya mpakani.
Alimtaka Waziri Lukuvi kutembelea eneo hilo ili
mgogoro uishe na wananchi wafanye kazi ya
uzalishaji.
Mbunge wa Karatu (Chadema), Willy Quambalo
alisema kuna mwekezaji katika wilaya hiyo
ambaye amepewa ekari 3,850 huku wananchi
wakipata shida kwa sababu ameziba njia ambayo
inapita katika eneo hilo.
Lukuvi amtaja Lowassa bungeni
Waziri Lukuvi amemgonganisha Mbunge wa
Monduli, Julius Kalanga na mtangulizi wake
Edward Lowassa, kuhusu shamba la Makuyuni
lililopo jimboni humo.
Lukuvi alifanya hivyo wakati akitoa majibu ya
hoja mbalimbali za wabunge kuhusu hotuba ya
bajeti yake, lakini Kalanga katika mchango wake
alilalamikia kuchelewa kwa utekelezaji wa
uamuzi wa Serikali wa kurejesha mashamba
makubwa kwa wananchi, likiwamo la Makuyuni.
Akijibu hoja hilo, Lukuvi alimwambia Kalanga
kuwa shamba hilo la Makuyuni litarudishwa kwa
wananchi, lakini itakula kwake kwa kuwa liko kwa
Lowassa.
“Rais Mkapa (Benjamin) aliamua shamba hilo
lirudi kwa wananchi na Lowassa ndiye aliyesaini
hati ya shamba hilo,” alisema Lukuvi.
Alisema kuwa atahitaji ushirikiano wa Kalanga na
halmashauri ya Monduli, kulikabidhi shamba hilo
kwa wananchi.
Wakati huo huo, Lukuvi amepiga marufuku watu
wote wenye mashamba makubwa ambao
wanayapima na kuuza viwanja, waache kwa
kuwa haliruhusiwi kuanzia sasa.
“Kama ni shamba litabaki kuwa shamba kama
mtu alinunua shamba anataka kubadilisha liwe
kiwanja imekula kwake,” alisema Lukuvi na
kuongeza kama kuna mtu anataka kufanya hivyo
akabidhi shamba kwa halmashauri ili ligawiwe au
kuuzwa.chanzo habar leo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top