Wafanyakazi wa kampuni ya kichina Hain international LTD wagoma.soma zaid.
Wafanyakazi wa kampuni ya kichina ya Hainan
International LTD inayojenga njia kuu ya umeme
kutoka Singida kwenda Shinyanga na kupanua
kituo cha kupoozea umeme cha Ibadakuli cha
Shinyanga mjini wameandamana hadi katika ofisi
ya idara ya kazi mkoani humo kudai mapunjo ya
mishahara yao ambayo wamekuwa
wakizungushwa kwa muda mrefu huku
wakishangazwa na tukio la kupewa barua za
kusimamishwa kazi wakati bado wanamdai
mwajiri.ITV ilipofika katika ofisi ya idara ya kazi mkoani
Shinyanga na kukuta maandamano ya
wafanyakazi hao huku wakidai kuwa wanaidai
kampuni zaidi ya shilingi milioni sitini za
kitanzania kama mapunjo ya mishahara yao hali
iliyomlazimu afisa kazi wa mkoa wa Shinyanga
Bw.Deogratius Mabula kuingilia kati na kutoa
maelekezo nini kifanyike ili kupata stahiki zao.
Naye msemaji wa kampuni hiyo Bi.Angel Julius
amesema ametoka Dar es Salaam kuja kuongea
na wafanyakazi na kuwajulisha kuwa kampuni
haijapata pesa za kuwalipa lakini anashangaa
kukuta wafanyakazi wamepewa barua za
kufukuzwa kazi hali ambayo hawezi kuwa na jibu
la kuwaambia.
Kwa upande wake katibu wa vyama vya
wafanyakazi mkoani Shinyanga Bw.Fabiani
Samkumbi amekiri kuwa wafanyakazi hao
wanaidai kampuni mapunjo ya mishahara ya
muda mrefu na makubaliano yalishafikiwa lakini
mambo yameenda kinyume huku mchina
anayesimamia mradi huo Bw.Zhao Chongring
akidai kuwa yeye hahusiki na mishahara ya
wafanyakazi lakini ofisi kuu iliyoko Dar es Salaam
ndiyo inayohusika na anafanya mawasiliano ili
kujua ni lini watalipwa pesa zao.chanzo itv
0 comments :
Post a Comment