Watanzia 8 waliotaka kujiunga na Al- shabab wakatwa kenya.soma zaid.
Serikali ya Kenya imefichua kwamba
imewakamata raia wanane wa Tanzania
waliokuwa katika harakati za kujiunga na kundi la
wapiganaji la al-Shabab nchini Somalia.
Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya
habari, polisi wanasema raia hao waliokamatwa
katika kipindi cha miezi miwili iliopita walikiri
kuwa mbioni kujiunga na kundi hilo la ugaidi.
Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya kundi la
watu wanaojidai kuwa wapiganaji wa Kiislamu
kuweka video mtandaoni likidai uwepo wa
wapiganaji wa Kiislamu nchini Tanzania
Video hiyo iliwaonyesha wanaume hao wakiwa
wamejifunika nyuso zao kwa vitambaa na
barakoa.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na
kuwahimiza Waislamu katika taifa hilo la Afrika
Mashariki kujiunga na kampeni yao.
Mkuu wa polisi Kenya amesema polisi pia
wametibua shambulio la Islamic State
Polisi wa Kenya pia wanasema wamefanikiwa
kutibua njama ya wanachama wa kundi linalojiita
Islamic State ya kutekeleza mashambulio nchini
humo na kuwakamata washukiwa wawili.
Wawili hao Kiguzo Mwangolo Mgutu na Abubakar
Jillo Mohammed walipewa mafunzo ya kuwa na
itikadi kali kabla ya kuingizwa katika kundi la IS
na Mohammed Ali aliyekamatwa awali na
ambaye anasaidia polisi na uchunguzi, polisi
wamesema.
Kulingana na taarifa hiyo, kufuatia kukamatwa
kwa Mohammed Ali, wafuasi wake wamekuwa
wakipanga kufanya mashambulizi ya kulipiza
kisasi sana wakilenga sekta ya uchukuzi wa
abiria.
Kukamatwa kwa wawili hao, kumezuia kutokea
kwa mashambulio katika miji ya Nairobi na
Mombasa.chanzo star vt.
0 comments :
Post a Comment