Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, May 25, 2016

Wewe mwananch unaamini huyu waziri magembe ni mzigo na ni mwepesi kama tishu?

Dodoma. Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema),
Ester Bulaya jana alichafua hali ya hewa bungeni
baada ya kusema kwamba Waziri wa Maliasili na
Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ni mzigo na
mwepesi kama ‘tishu’ kwa sababu hana uwezo
wa kusimamia mambo mazito yaliyopo katika
wizara hiyo, kama vile migogoro ya wananchi na
hifadhi za Taifa.
“Huyu waziri ni mzigo kama alivyowahi kusema
(Abdulrahman) Kinana. Mimi nasema yeye ni
mwepesi kama tishu, hawezi kuisaidia wizara hii
nyeti,” alisema mbunge huyo jana wakati
akichangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na
Utalii.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na
Bunge, Jenista Mhagama alisimama na kuomba
mwongozo wa mwenyekiti juu ya mbunge huyo
kutumia maneno ya kuudhi ambao uliungwa
mkono na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge
aliyemtaka Bulaya kufuta neno mwepesi kisha
aendelee na hotuba yake. Hata hivyo, Bulaya
alikataa kufuta neno hilo na kusema wabunge
hawaamuliwi maneno ya kutumia.
Chenge aliendelea kumsihi mbunge huyo kufuta
neno hilo na katika mabishano hayo yaliyodumu
kwa dakika tatu, baadaye, Bulaya alikubali
kuondoa neno ‘tishu’ na kuliacha neno mwepesi
na kuruhusiwa kuendelea kuchangia.
“Mwenyekiti sitafuta neno mwepesi, kama neno
‘tishu’ linawakera basi naliondoa libaki mwepesi,”
alisema Bulaya.
Katika mchango wake, Bulaya alisema wananchi
wanaoishi katika hifadhi zilizopo jimboni mwake
wananyanyaswa na askari wanyamapori wakati
Serikali imeshindwa kuwatengenezea mazingira
mazuri ya kuishi.
Alimtaka waziri huyo kushughulikia kero zote
zinazowakabili wananchi wa Bunda akisema
Serikali haiendeshwi kwa maneno matupu, bali
vitendo na dhamira ya dhati ya kuwahudumia
wananchi.
“Tatua matatizo jimboni kwangu ili niweze
kukupima kama wewe ni mzito au mwepesi,”
alisema mbunge huyo akimwambia Profesa
Maghembe.
Baada ya Bulaya kumaliza muda wake, mbunge
aliyefuatia alikuwa Abdallah Ulega wa Mkuranga
(CCM) ambaye alisema kuna haja ya wabunge
kupimwa kama wamelewa getini ili kujua akili
zao.
“Kijana aliyefunzwa vizuri hawezi kumtukana
mzee kama yule (Maghembe). Kama suala ni
uwaziri basi aangalie hata umri wake kabla ya
kuzungumza... Naungana na aliyesema wabunge
tupimwe vilevi kabla hatujaingia humu ndani.
Unaweza kujenga hoja yako bila kutukana,
huhitaji kutukana ili waziri atekeleze madai
yako,” alisema mbunge huyo.chanzo mwananch.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top