Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 26, 2016

Wavuvi wagoma mwanza kisa wananyanyaswa na mabosi wao.

Zaidi ya wavuvi 1,000 wa kisiwa cha Kasarazi
wilaya ya Sengerema mkoani
mwanza,wamegoma kufanya kazi kwa siku ya
nne mfululizo wakipinga vitendo vya
unyanyasaji,ikiwemo kunyimwa chakula
vinavyodaiwa kufanywa na wamiliki wa
mitumbwi,huku uongozi wa serikali wilayani humo
ukilalamikiwa kwa kufumbia macho vitendo hivyo
vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Katibu wa umoja huo wa wavuvi wapatao 1,165
waliopo katika kisiwa cha Kasarazi halmashauri
ya wilaya ya Buchosa Boniphace Mgeta
amesema wameamua kugoma kuingia ziwani
kuendelea na shughuli zao za uvuvi kwa madai
ya kunyanyaswa na matajiri hao,huku mkuu wa
wilaya hiyo Zainab Talack akishindwa kuupatia
ufumbuzi mgogoro huo licha ya kukutana na
pande hizo mbili ofisini kwake .
Uongozi wa wamiliki wa vyombo vya uvuvi wa
kisiwa hicho cha Kasarazi kilichomo ndani ya
Ziwa Victoria, kupitia kwa katibu wao Msilikale
Juma amesema chanzo cha mgogoro huo
ulioanza kufukuta kuazia mwezi Aprili mwaka huu
ni hujuma inayodaiwa kufanywa na baadhi ya
wavuvi wasio waaminifu na kusababisha hasara
ya mamilioni ya shilingi kwa wamiliki wa vyombo
vya uvuvi.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Zainab talack
akizungumza kwa njia ya simu kutokea
wilayani Sengerema amekiri kuutambua mgogoro
na kuzitaka pande zote mbili kukaa chini na
kufanya mazungumzo yenye lengo la kufikia
mwafaka.chanzo itv

0 comments :

Post a Comment

Back To Top