Watunishi hewa wayaponza mabenki.soma zaid
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda ametoa siku 21 kwa benki zilizokuwa
zikitumika kuweka mishahara ya watumishi hewa,
kurejesha fedha hizo serikalini ; au kubainisha
waliokuwa wakitumia akaunti hizo, kuchukua
fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Makonda alisema benki ndio pekee wanaoweza
kusaidia mkoa, kutambua wahusika waliokuwa
wanatumia akaunti hizo pamoja na wale
waliokuwa wanachukua fedha hizo.
Alisema watu hao wasipopatikana, inamaanisha
fedha bado zipo katika benki hizo, hivyo
zinapaswa kuzirudisha serikalini zifanye
maendeleo kwa wananchi. “Tayari
tumeshaziandikia benki hizo barua na kuwapatia
majina na akaunti na kuwataka kutuwasilishia
majina ya wahusika, waliohusika na akaunti hizo
ili kusaidia kutambua mtandao mzima wa
wahusika wa suala la watumishi hewa ambao
wameigharimu serikali,” alisema Makonda.
Alitaja benki hizo pamoja na fedha wanazodai
kuwa ni benki ya NMB ambayo inadaiwa zaidi ya
Sh bilioni mbili, CRDB zaidi ya milioni 400, NBC
zaidi ya milioni 141, DCB milioni 85, Standard
Chartered zaidi ya Sh milioni mbili na Community
Benki zaidi ya milioni 100.
“Hakuna mtu anayeweza kutumia akaunti ya mtu
bila kufuata taratibu za kibenki, hata kama mtu
amefariki kuna taratibu za kufuata ndipo apate
akaunti, naamini benki hizi zitasaidia
kuwatambua wahusika wote,” alisisitiza.
Aidha, alizitaka benki hizo kufunga huduma za
akaunti hizo ;na zisifanye malipo yoyote mpaka
fedha hizo zitakapopatikana. Mpaka sasa, Mkoa
wa Dar es Salaam umebainika kuwa na
watumishi hewa 283, ambao wanadaiwa
kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 3.6
ambazo zilitumika kuwalipa mishahara.
0 comments :
Post a Comment