Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, June 1, 2016

Donard Trump aendelea kujizolea umaarufu na kukubalika na nchi nyingine.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini
vimemsifu mgombea wa urais kupitia tiketi ya
chama cha Republican Donald Trump kuwa
mwanasiasa ''mwenye hekima'' ambaye anaweza
kuwa na ushirikiano mzuri na Korea Kaskazini.
Uhariri wa mtandao wa DPRK ulisema kwamba ni
mgombea ''anayeona mbali''.
Bw Trump hivi majuzi alisema kuwa alikuwa
tayari kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini
Kim Jong Un na pia amependekeza kuviondoa
vikosi vya Marekani kutoka Korea Kusini.
Wachanganuzi wanasema uhariri huo sio sera
rasmi ya taifa hilo lakini huenda unaangazia fikra
za Pyongyang.
BBC Monitoring imesema kuwa DPRK ni
miongoni mwa mitandao ya propaganda
inayotumiwa na Korea Kaskazini.
Mtandao huo unadaiwa kuwakilisha maoni ya
Pyongyang lakini mwandishi wake hajulikani.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top