Upinzani wamewasilisha kwa sipka wa bunge hoja kumwondoa Naibu spika.soma zaid.
Upinzani
wamewasilisha kwa Spika
wa Bunge hoja ya
kumwondoa madarakani
Naibu Spika, Dk Tulia
Ackson kwa kutokuwa na
imani naye.
Hatua hiyo imefikiwa na
wabunge hao kufuatia
kutoridhishwa na
mwenendo wa uongozi wa
Dk Tulia anapokalia kiti cha
Spika.
Tangu Jumanne wiki hii,
wabunge hao wamekuwa
wakisusa vikao
vinavyoongozwa na
kiongozi huyo kwa madai
anaminya demokrasia.
Walifikia uamuzi huo baada
ya Dk Tulia kuzuia
kujadiliwa hoja ya
kufukuzwa kwa wanafunzi
zaidi ya 7,000 wa Chuo
Kikuu cha Dodoma (Udom)
iliyowasilishwa na Mbunge
wa Arumeru Mashariki,
Joshua Nassari na
kukatisha mjadala wa
bajeti ya maji.
Kitendo hicho kiliwafanya
wabunge wote wa upinzani
kupingana na maamuzi ya
Dk Tulia, jambo
lililosababisha watolewe
bungeni.
Kutokana na hali hiyo
wabunge hao kupitia
Mbunge wa Simanjiro,
James Ole Millya
akisindikizwa na Mbunge
wa Kibamba, John Myika
wa Chadema na Mbunge
wa Konde wa CUF, Khatibu
Said Haji waliwasilisha hoja
hiyo kwa Katibu wa Bunge,
Dk Thomas Kashilillah
baada ya Spika, Job
Ndugai kutokuwapo
bungeni.
Hoja hiyo iliwasilishwa kwa
mujibu wa Kanuni ya 138
(1) ambayo inaeleza
utaratibu wa jinsi ya
kumwondoa Naibu Spika.
Kanuni hiyo inasema,
“Utaratibu wa kumwondoa
Naibu Spika madarakani
chini ya Ibara ya 85(4)(c)
ya Katiba utakuwa kama
ule wa kumwondoa Spika,
isipokuwa tu taarifa ya
kusudio la kumwondoa
Naibu Spika madarakani
inayoeleza sababu kamili
za kuleta hoja hiyo,
itapelekwa kwa Spika
ambaye ataiwasilisha
kwenye Kamati ya Haki,
Maadili na Madaraka ya
Bunge kwa ajili ya
kuijadili.”
Fasili ya pili ya Kanuni hiyo
inasema: “Endapo Kamati
ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge
itaridhika kuwa zipo
tuhuma mahususi dhidi ya
Naibu Spika zinazohusu
uvunjaji wa Katiba, Sheria
au Kanuni zinazoongoza
Shughuli za Bunge, basi
Kamati hiyo itaidhinisha
kuwa hoja hiyo ipelekwe
bungeni ili iamuliwe.”
Kwa mujibu wa Ibara ya
85(4)(c), Naibu Spika
atakoma kuwa Naibu Spika
na ataacha kiti cha Naibu
Spika endapo ataondolewa
kwenye madaraka ya Naibu
Spika kwa azimio la Bunge.
Akizungumzia uwasilishwaji
wa hoja hiyo, Millya
alisema taarifa zaidi
watatoa leo kuhusu
msimamo wao huo.
Dk Tulia aliwataka
wabunge wenye
malalamiko juu ya utaratibu
wa uendeshaji wa shughuli
za Bunge kukata rufaa kwa
kufuata Kanuni za Bunge.
Alisema kanuni ndogo ya
5(2) inasema Spika
atawajibika kutilia nguvu
kanuni zote za Bunge na
5(3) inasema Spika
anaweza kumtaka mbunge
yeyote anayekiuka kanuni
hizi kujirekebisha mara
moja.
Alisema kwa hiyo mbunge
yoyote asiyeridhika, kanuni
za Bunge zinamruhusu
kukata rufaa na
zinamweleza nini cha
kufanya.
Je, Una
Habari,Picha,Tang
azo,Makala,
Ushauri n.k.?Basi
Wasiliana Nasi
Simu/WhatsApp
0757478 553 ,0625
918 527
Hifadhi blog hii
kwenye simu yako
ili upate habari
zetu kwa urahisi
zaidi Bofya HAPA
U Download sasa
App ya Malunde1
blog
Malunde
Like Page
Facebook Blogger Plugin by
Labels: siasa
- Print Email
×
02
Jun 2016
Share to:
Previous
Jambazi
Auawa
Akipamba
na na
Polisi Jijini
Mwanza
Rais Magufuli Amteua
Anne Makinda Kuwa
30 May 2016
Search
0 comments :
Post a Comment