Watumishi 5 wasimamishwa kazi wilayani nzega mkoani tabora.soma zaid.
BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Wilaya
ya Nzega, mkoani Tabora limewasimamisha kazi
watumishi watano kwa tuhuma za ubadhirifu wa
zaidi ya Sh milioni 190, ambazo ni fedha za
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) pamoja na fedha
za chanjo.
Watumishi hao wanatuhumiwa kughushi nyaraka,
kukosekana kwa baadhi ya nyaraka za fedha,
kuidhinisha malipo hewa pamoja na kukiuka
taratibu na kanuni za utumishi wa umma na
kukiuka matumizi ya fedha za umma.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa
Tabora, Aggrey Mwanri na Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo, Kiwelle Bundala. Kiwelle
aliwataja watumishi waliosimamishwa kazi
kupisha uchunguzi kuwa ni Katibu wa Afya
Wilaya, Kisasu Sikalwanda, Mhasibu wa
Halmashauri ya Wilaya, Denins Gombeye, Mratibu
wa Chanjo wa Wilaya, Joel Mjondela, Mganga
Mkuu Hospitali ya Wilaya, Emmanuel Mihayo na
Mweka Hazina, Stanslaus Kalokola.
Alisema uchunguzi utakapofanyika na kubaini
watumishi hao hawana hatia wataendelea na kazi
na ikiwa tofauti hatua nyingine za kinidhamu
zitachukuliwa.
Mwanri alilipongeza baraza hilo kwa kuchukua
maamuzi magumu ya kulinda maslahi ya
wananchi na kuongeza kuwa ataendelea
kusimamia sheria na taratibu za utumishi wa
umma. Aliwataka watumishi wa Serikali
kuhakikisha wanasimama katika nafasi zao za
kufanya kazi kwa uandilifu na kuepuka ubadhirifu
ambao hauna faida ndani yake.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), Mkoa wa Tabora, Mohamed Msangi
alisema sababu za watumishi hao kusimamishwa
kazi ni kughushi nyaraka za malipo, kukosekana
kwa baadhi ya nyaraka pamoja na kufanya
malipo hewa.
Alisema taarifa ya CAG inaonesha kukiuka
taratibu nyingi za matumizi ya fedha za umma.
0 comments :
Post a Comment