Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, June 1, 2016

Wabunge wa upinzani waliosimamishwa watakutana na kitanzi kingine.

Wabunge saba wa upinzani waliosimamishwa
bungeni, watakumbana na kibano kingine cha
kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote
cha kutumikia adhabu.
Dodoma. Wabunge saba wa upinzani
waliosimamishwa bungeni, watakumbana na
kibano kingine cha kukatwa mshahara na posho
kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.
Wabunge hao ambao Jumatatu walisimamishwa
kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda tofauti
kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe
(Kigoma Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki),
Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini)
, John Heche (Tarime Vijijini) na Godbless Lema
(Arusha Mjini).
Adhabu hiyo ilitolewa kama azimio la Bunge
baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka
ya Bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe
kutokana na kuomba mwongozo wa kiti cha
Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa
uamuzi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top