Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, June 1, 2016

Watuhumiwa 6 wa ubakaji morogoro wanyimwa dhamana mahakamani.soma zaid.

Washtakiwa sita wanaokabiliwa na
makosa tofauti yakiwemo ya kubaka,
kulawiti na kusambaza picha chafu na za
ngono wameendelea kusota rumande kwa
kukosa dhamana, baada ya mvutano mkali
wa mawakili wa upande wa mashtaka na
upande wa washtakiwa kuibuka
mahakamani hapo, na hakimu
anayesikilisha shauri la dhamana
kuahirisha shauri hadi Juni 15 mwaka
huu kutoa uamuzi juu ya dhamana.
Miongoni mwa washtakiwa hao,
wawili,Iddi Adam Mabena (21) mkazi wa
Njombe na Zuberi Thabit (30) mkazi wa
Mbarali Mbeya wanaokabiliwa na shtaka
la kumbaka na kumlawiti binti mwenye
umri wa miaka 21 mkazi wa Wami
Dakawa,wilayani Mvomero wanalodaiwa
kutenda Aprili 27 mwaka huu majira ya
usiku katika nyumba ya kulala wageni ya
titii iliyopo wami dakawa wilayani
mvomero,shauri lao linalosikilizwa faragha
limeahirishwa tena mbele ya Hakimu
mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya mkoa
wa Morogoro Mary Moyo.
Upande wa mashtaka katika shauri hilo
linalosikilizwa faragha kwa mujibu wa
sheria, umewakilishwa na waendesha
mashtaka Gloria Rwakibalila,Edgar
Bantulaki,Calistus Kapinga na Mohamed
Mkali na limepangwa kufikishwa tena
mahakamani hapo Juni 15 mwaka huu
kwaajili ya kuanza usikilizwaji wa awali
baada ya upelelezi kukamilika.
Uamuzi wa dhamana itolewe ama
isitolewe umeshindwa kufikia muafaka
baada ya mvutano wa kisheria wa
mawakili wa utetezi na wa Jamhuri, katika
shtaka la kusambaza picha chafu na za
ngono kwa njia ya mtandao kinyume na
sheria ya makosa ya mtandao no 14 ya
mwaka 2015, linalosikizwa mbele ya
hakimu Ivan Msaki,wa Mahakama ya
Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro,dhidi
ya washtakiwa sita,iddi Mabena na Zuberi
Thabit,wanaotetewa na wakili Mohamed
mkali,na Rajab Salehe,Ramadhani Ally
Makunja, Muhsin Ngai na John Peter
Thabiti maarufu kama paroko, wakazi wa
wami dakawa wilayani Mvomero
wanaotetewa na wakili Ignas Punge.
Upande wa mashtaka umeendelea kutetea
uamuzi wake wa kuwasilisha kiapo cha
kupinga dhamana kwa vile shauri hilo
limevuta hisia ya watu, usalama wao
utakuwa mashakani wawapo uraiani hasa
ikizingatiwa wanadaiwa kudhalilisha utu
wa mwanamke na kutoharibu upelelezi
kwa vile bado haujakamilika,na kwamba
taarifa za kiintelijensia zimebainisha
wakiachiwa huru wanaweza wakadhuriwa
na jamii.
Hata hivyo upande wa utetezi
uliowasilisha hati kupinga kiapo hicho
umedai dhamana ni haki ya
mshtakiwa,hakuna raia aliyewasilisha
kiapo kuhusu hasira kali alizonazo dhidi
ya washtakiwa isipokuwa labda ni hisia za
mkuu wa upelelezi wa mkoa.
Hakimu Ivan Msaki ameahirisha shauri
hilo hadi Juni 15 mwaka huu ambapo
uamuzi wa washtakiwa kupewa dhamana
au kunyimwa dhamana utajulikana.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top