Donard Trump na Hilarly clinton watupiana vijembe vya maneno.soma zaid.
Mgombea anayetarajiwa kuteuliwa wa chama
cha Republikan hapa Marekani, Donald Trump,
Alhamisi usiku alimjibu vikali mgombea
anayeongoza wa tikiti ya Demokratik, Hillary
Clinton, kufuatia hotuba juu ya sera za kigeni
aliyoifanya waziri huyo wa zamani wa mambo ya
nje.
Clinton alimshambulia kwa maneno makali
Trump, na kumtaja kama asiye na fikra timamu
za kuongoza Marekani huku akisema kazi hiyo,
inahitaji ujuzi, uthabiti na uwajibikaji mkubwa.
Lakini Trump alimjibu kwa kusema kuwa fikra
zake ni timamu kuliko za Clinton. Trump,
aliyekuwa akizungumza mjini San Jose,
California, alisema Hilary ni mdanganyifu na
kwamba hakusema ukweli kuhusu sera ambazo
Trump amekuwa akisema angezingatia endapo
atachaguliwa kuwa rais.
Kabla ya Trump kutoa hotuba yake, Clinton
alisisitiza kwamba ana uzoefu mwingi alioupata
kama mke wa rais, kama seneta na kama waziri
wa mambo ya nje wa Marekani, na kuongeza
kuwa angetoa mwelekeo dhabiti wa kidiplomasia
ambao unahitajika na Marekani.
0 comments :
Post a Comment