Breaking News
Loading...

Advert

Friday, June 3, 2016

Hizi ni tetesi za usajili barani ulaya, poul pogba kutua man city? .soma zaid.

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 03.06.2016
Usajili wa kiungo wa Ujerumani Ilkay Gurdogan,
25, ni mwanzo tu wa usajili mkubwa wa meneja
mpya wa Man City Pep Guardiola, ambaye
huenda akatumia pauni milioni 250 (Daily Mirror),
Man City pia wako tayari kutoa pauni milioni 39
kumsajili beki kutoka Ufaransa Aymeric Laporte,
22, kutoka Athletic Bilbao (Guardian), Guardiola
anataka kusajili wachezaji wengine sita,
wakiwemo Toni Kroos, 26, kutoka Real Madrid, na
kiungo wa Juventus Paul Pogba, 23 (Manchester
Evening News), Manchester United wamepanda
dau ambalo ni rekodi ya Uingereza ya pauni
milioni 60 kumtaka kiungo kutoka Ufaransa, Paul
Pogba, aliyeondoka Old Trafford kwenda
Juventus mwaka 2012 (Sun), mabingwa wa
Ufaransa Paris St- Germain wako tayari kutoa
pauni milioni 46 kumsajili kiungo mshambuliaji wa
Liverpool Phillipe Coutinho, 23, (Le 10 Sport),
PSG wamezungumza na wawakilishi wa
Coutinho, lakini bado hawajapata dau rasmi
(Liverpool Echo), Everton wanmtaka meneja wa
Southampton, Ronald Koeman pamoja na Monchi
ambaye ni mkurugenzi wa michezo wa Sevilla
(Liverpool Echo), Everton wanataka kumfanya
Ronald Koeman meneja anayelipwa zaidi katika
EPL (Daily Mail), Dani Alves ameonekana jijini
Paris na kuzua tetesi kuwa huenda akajiunga na
PSG (Daily Express), hata hivyo taarifa nyingine
zinasema Alves atajiunga na Juventus (Marca),
Tottenham wamempa mkataba mpya Harry Kane
wa pauni 100,000 kwa wiki na kumfanya
mchezaji anayelipwa zaidi Spurs, huku Man Utd
wakimnyatia (Squawka), mshambuliaji wa Real
Madrid Cristiano Ronaldo, 30, ametoa sadaka
takriban pauni 500,000- kitita chake cha ziada
cha ushindi wa Champions League (Sun), kiungo
wa Juventus Kwadwo Asamoah, 27, anataka
kuhamia Chelsea (Bleacher Report), mkurugenzi
wa michezo wa Besitkas amethibitisha kuwa
klabu hiyo inamtaka kipa wa Arsenal David
Ospina, 27 (Daily Express), Leicester City
wameanza mazungumzo na kipa wake Kasper
Schmeichel ya kumpa mkataba mpya wa miaka
mitano (Daily Mail), Alvaro MOrata, anayesakwa
na Arsenal amewaambia Real Madrid kuweka
wazi mustakbali wake (Daily Mirror), Chelsea
wanamtaka mshambuliaji wa Liverpool, Christian
Benteke, 25, iwapo watashindwa kumrejesha
Romelu Lukaku Stamford Bridge (The Times).

0 comments :

Post a Comment

Back To Top