Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, June 5, 2016

Rais magufuli aendelea kuungwa mkono kwa hatua mbalimbali anazozichukua hapa nchini.soma zaid.

MTANDAO wa Wanafunzi Nchini (TSNP)
umemuunga mkono Rais John Magufuli kwa
kuwachukulia hatua za kuwawajibisha
waliohusika kuwadahili wanafunzi wasio na sifa
katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Aidha, mtandao huo umeishauri serikali kusitisha
programu maalumu ya kusomesha walimu wa
masomo ya sayansi ili kutoa fursa kwa
wanafunzi waliodahiliwa kumaliza masomo yao
na pia serikali kupanga utaratibu mpya.
TSNP pia imeiomba serikali kuwaruhusu
wanafunzi ambao wamebakiza mwaka mmoja wa
kumaliza masomo yao ya Stashahada (Diploma)
waendelee na masomo yao. Hayo yameelezwa na
Katibu Mkuu wa mtandao huo, Alphonce Lusako
katika mkutano wa kutoa tamko la mtandao huo
pamoja na la wanafunzi waliofukuzwa UDOM.
Lusako alisema, hatua hiyo haiepukiki kutokana
na wahusika kudahili kinyume na vigezo
vilivyowekwa na serikali. Aidha, alisema mtandao
huo ulikuwa ukifanya utafiti wa kina kupitia Idara
ya Tafiti na Mafunzo ya mtandao huo kuhusu
sakata hilo.
Alisema serikali ilianzisha programu hiyo kwa
lengo la kutatua uhaba wa walimu wa masomo
ya sayansi na kuwekwa sifa za udahili, lakini
hatimaye Waziri mwenye mamlaka aliondoa na
kuongeza kuwa ikitokea mwanafunzi au kundi la
wanafunzi halitapewa haki zao, mtandao huo
utashirikiana na wadau wa elimu zikiwemo Asasi
za kiraia kufungua kesi mahakamani ili kudai haki
zao.
Akisoma taarifa rasmi ya wanafunzi
waliosimamishwa UDOM, Gibson Johnson
alisema, wanaiomba serikali kuangalia
uwezekano wa wao kuendelea na masomo yao.
“Tunaiomba na kuililia serikali iangalie wale
wenye division I, II na III ituache tumalizie
masomo yetu, lakini watakaokuwa na ufaulu wa
chini kuanzia division IV itafute namna ya
kuwasaidia,” alisema Johnson.
Wamemuomba Rais Magufuli na Waziri wa Elimu,
Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako kuona haja ya
kuwarudisha chuoni ili kumaliza masomo yao
kama ilivyopangwa, kama jambo hilo
likishindikana serikali ifanye mkakati wa
kuwatafutia vyuo stahiki ili wamalize masomo
yao.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top