Breaking News
Loading...

Advert

Monday, June 27, 2016

Kipaji cha mpira champeleka ughaibuni.soma zaid.

Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola,
Mariam Sezinga, akizungumza na
waandishi wa habari kuwaelezea juu ya
safari ya mchezaji Musa Said anayetarajia
kuondoka Jumatano ya Juni 28, 2016
kwenda nchini Ufaransa kwenye kambi ya
kimataifa ya Copa Coca-Cola. Pembeni ni
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, Mchezaji
Musa Said Bakari na Mwalimu wake wa
Kibasila
MCHEZAJI bora wa mashindano ya
UMMISETA yaliyofanyika mwaka jana
mkoani Mwanza, Said Musa Jumatano ya
Juni 28, 2016 kuelekea Ufaransa katika
kambi ya Kimataifa ya Copa Coca - Cola
ambayo imeandaliwa na kampuni ya
kinywaji cha Coca - Cola . Akizungumza
jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
Mohamed Kiganja alisema udhamini wa
kampuni ya Coca - Cola imetambua
umuhimu wa michezo hivyo kukubali
kudhamini michezo kupitia shule za
sekondari ili kukuza vipaji vya
wanamichezo chipukizi ambao
wanamalengo makubwa katika kuitumikia
nchini yao kupitia michezo. “Kwetu sisi
imekuwa faraja kwa kuibua kipaji
kichanga ambacho kitakuwa ni mfano wa
kuigwa kama ilivyo kwa Samatta ambaye
amekuwa kioo kwa jamii ya wanamichezo
na hivyo kuomba makampuni mengine
kujitokeza kwa ajili ya kusaidiana na Coca
- Cola”, alisema. Kiganja alimtaka Musa
kuzingatia nidhamu kipindi chote
atakachokuwepo kwenye kambi ili
kujijengea heshima katika kukuza kipaji
chake kwa kipindi chote ambacho atakuwa
chini ya walimu wageni ambao hajawahi
kukutana nao na hiyo italeta heshima
nchini. Kwa upande wa Meneja msaidizi
wa chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga,
alisema wamefurahi kupata nafasi ya
kudhamini mashindano hayo kwa kuwa
ndiyo mara yao ya kwanza na
imefanikiwa kufikia malengo ya kupata
mchezaji ambaye atakuwa muwakilishi wa
Tanzania katika kambi ya Kimataifa ya
Copa Coca - Cola iliyopo jijini Paris nchini
Ufaransa. Alisema Musa ataondoka kwa
kupitia Nairobi kwa kuwa kozi inaanza
kesho na kumalizika Julai 4, hivyo
aliwataka wanafunzi wengine kujituma ili
kufikia malengo kama aliyofikia Mussa.
“Sisi kama kampuni imekuwa ni faraja
kwani tutakuwa tumeitangaza nchini kwa
kupitia Mussa na hii itakuwa ni
muendelezo katika michezo
inayoendelea,”alisema. Mussa ni
mwanafunzi wa shule ya sekondari
Kibasila ambaye alizaliwa Agosti 11, 2000
huku akiwa ni mchezaji tegemeo katika
timu ya shule na Mkoa wa Temeke ambapo
walitumia jina hilo kwa kupitia michezo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top