Mtu mmoja mkoani kigoma ajinyonga kwa wivu wa mapenzi.soma zaid.
Kigoma
Mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la
Norbert Gidion (30) mkaazi wa Masanga
katika Manispaa ya Kigoma
Ujiji amekutwa amefariki dunia akiwa
amejinyonga kwenye mti wa mwembe kwa
kile kinachosadikika kuwa ni wivu wa
mapenzi
Kamanda wa polisi mkoani kigoma Afande
Ferdinand Mtui, amethibitisha tukio hilo
na kusemw kwamba upelelezi wa awali
unaonesha kuwa chanzo cha kifo cha
Marehemu Norbert Gidion ni kutokuwepo
na maelewano dhidi ya marehemu na
mke wake, Bi.Happyfania Caristus.
"Natoa wito kwa wananchi kuacha
kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa
mazingira kama hayo husababisha
kutokea vifo visivyotarajiwa kwa jamii:,
alisema Kamanda Mtui.
Wakielezea tukio hilo wapangaji wenzie
marehemu wamesema kuwa kwa kipindi
kirefu marehemu alikuwa safari hadi
umauti unamkuta na kwamba hata
alivyorudi safari alikuwa halali nyumbani
kwa mke wake.
Mzazi wa marehemu Bw. Gidioni Hungu
amesema kuwa mazingira ya kifo hicho
imekuwa sintofahamu kwani alikuwa hana
maelewano mazuri na mkewe.
0 comments :
Post a Comment