Kujiondoe kwa uingereza EU kwa endelea kutikisa dunia.soma zaid.
Mzozo unaoikumba Uingereza ulionekana
kuongezeka Jumatatu huku maafisa wa Umoja
wa Ulaya wakitafuta mbinu za kukabiliana na
wasiwasi uliokithiri baada ya wapiga kura wa
nchi hiyo kuamua kwamba wataondoka Umoja
wa Ulaya, hatua ambayo imeitumbukiza
Uingereza katika hali ambayo imetajwa na
wengine kama iliyo mbaya zaidi tangu vita vya
pili vya dunia.
Katika jitihada za kusitisha kuyumbayumba katika
masoko ya fedha hii leo, Waziri wa Fedha wa
Uingereza, George Osborne, alitoa taarifa
mapema leo, iliyosema kuwa uchumi wa
Uingereza una nguvu na kwamba nchi hiyo iko
ytayari kufanya biashara na mataifa mengine.
George Osborne
Masoko ya bara Ulaya yalionekana kuathirika leo
asubuhi, hata ingawa hayakupata pigo kama
ilivyokuwa siku ya Ijumaa wakati ambapo soko la
fedha la London liliteremka hadi asilimia nane
kabla ya kuimarika kidogo na kusimamia kwa juu
kidogo ya asili mia tatu. Pauni ya Uingereza pia
ilianguka tena wakati wa soko ya mapema leo.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani, John Kerry, anazuru miji ya Brussels
na London hii leo, safari ambayo itakuwa ya
kwanza kwa afisa wa ngazi za juu wa serikali ya
Marekani katika miji hiyo miwili, tangu Uingereza
kupiga kura ya kujitenga na Umoja wa Ulaya wiki
jana, hatua ambayo imeleta wasiwasi mwingi kwa
Washington.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa Kerry,
ambaye ameongeza miji hiyo miwili kwenye
ratiba yake ya safari, ambayo awali ilikuwa
impeleke mjini Rome, ataelezea uungaji mkono
wa Marekani kwa Uingereza, na kusisitiza
umuhimu wa mataifa mengine wanachama wa
Umoja wa Ulaya, kusalia kwenye muungano huo.
Kerry alisema jana Jumapili kwamba Marekani
inasikitishwa na kura hiyo ya Uingereza kuondoka
kwenye Umoja wa Ulaya, lakini akaapa
kwendelea na uhusiano wa karibu na na umoja
huo ambao hivi karibuni utakuwa na mataifa 27
wanachama.
0 comments :
Post a Comment