Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 30, 2016

Lissu aachiwa kwa dhamana.soma zaid.

Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya
kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo
kudharaulisha watanzania dhidi ya
mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Lissu alisomewa mashtaka katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam leo Juni 30, 2016.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili
wa Serikali Mkuu Bernad Kongola
akisaidiana na Mawakili wa Serikali
Waandamizi, Nassoro Katuga na Salum
Mohammed.
Kongola alidai kuwa Juni 28,2016 eneo la
Mahakama ya Kisutu Ilala Dar es Salaam
mshtakiwa kwa nia ya kushawishi na
kudharaurisha watanzania dhidi ya
mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Alinukuu maneno ya Lissu
kwamba"Mamlaka ya Serikali mbovu ya
kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na
kila mtanzania kwa nguvu zote, huyu
dikteta uchwara lazima apingwe kila
sehemu kama uongozi utafanywa na
utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya
giza nene"
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.
upande wa jamhuri ulidai upelelezi
umekamilika na uliomba tarehe ya
kusikilizwa maelezo ya awali.
Upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la
mawakili 11 akiwemo Michael Ngalo, Peter
Kibatala na wenzao uliomba dhamana
kwa mshtakiwa kwa kuwa ni mbunge
atakuwa mwaminifu hataacha kufika
mahakamani.
Hakimu Yongolo alisema mshtakiwa
atakua nje kwa dhamana kwa kuwa na
wadhamini wawili watakaosaini hati ya
dhamana ya sh milini 2.
alitimiza masharti atasomewa maelezo ya
awali Agosti 2,2016.chanzo michuzi blog.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top