Madiwani washangazwa dereva kukusanya mapato ya kituo cha hospital.soma zaid.
Upungufu wa watumishi katika kituo cha afya cha Likombe manispaa ya Mtwara Mikindani kimepelekea dereva wa kituo hicho Ally Mchanyambi kutumika kukusanya mapato ya kituo, hali iliyowashangaza madiwani wa halmashauri hiyo na kutoa agizo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo kumuondoa kwenye nafasi hiyo mara moja na nafasi ijazwe na mtumishi mwenye sifa za uhasibu . Tatizo hilo limebainika katika kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichokuwa kikiwasilisha ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali manispaa ya Mtwara Mikindani. Akizungumza mara baada ya baraza hilo kumalizika mstaiki meya wa manispaa hiyo Geofrey Mwanchisye amesema wamelazimika kufanya hivyo baada ya ripoti hiyo kubaini nafasi hiyo ya dereva inaweza kusababisha upotevu wa mapato na uwekaji mbaya wa hesabu. Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego pamoja na mkuu wa wilaya ya Mtwara Fatuma Ally walionyesha kusikitishwa na kitndo hicho. ilipojaribu kumtafuta mkurugenzi wa manipaa hiyo Ambakisye Shimwela ambaye hakuwepo ofisini simu yake iliita bila kupokelewa. Hata hivyo kwa mujibu wa diwani wa kata ya Likombe Muksini Komba ambaye yuko nje ya mkoa amesema kutokana na ukusanyaji mbovu wa mapato kituo hicho kinashindwa kununua dawa za kutosheleza mahitaji.chanzo itv
0 comments :
Post a Comment