Breaking News
Loading...

Advert

Monday, June 20, 2016

Al shabab wamewauwa polisi 5 wa kenya mjini Mandera.

Maafisa 5 wa polisi wa Kenya wameuawa mapema leo mjini Mandera katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al shabab kutoka Somalia. Kamishna wa jimbo hilo la kaskazini mashariki mwa Kenya bwana Job Borongo ameithibitishia BBC kuwa wapiganaji hao walifanya shambulizi la kuvizia dhidi ya msafara wa magari ya polisi uliokuwa ukienda El Wak wakitumia guruneti. Maafisa hao tano waliangamia papo hapo huku gari walimokuwa wakisafiria likiharibiwa kabisa. Maafisa wengine wanne wamejeruhiwa vibaya. Msafara huo wa polisi ulikuwa ukitoa ulinzi kwa msafara wa mabasi ya uchukuzi wa umma, desturi iliyoanzishwa baada ya wapiganaji hao kuteka basi moja na kuua abiria 28 wakristu. Gavana wa Mandera bwana Ali Roba aliwalaumu maafisa wa polisi katika eneo hilo kwa kupuuza tahadhari iliyotolewa na wenyeji kuhusiana na mashambulio ya kigaidi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top