Ukawa leo waja na saili mpya bungeni.soma zaid.
LEO wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) wametibua taratibu
za Bunge kwa mara nyingine, anaandika Faki
Sosi.
❝
Wametoka nje baada ya Dk. Tulia Ackson,
Naibu Spika wa Bunge kuongoza Bunge hilo,
hatua hiyo ni mwendelezo wa kupinga
kuhudhuria vikao hivyo kuongozwa na
kiongozi huyo.
Hata hivyo, mtindo wa leo wa Ukawa umekuwa
tofauti na siku zote hususani katika mavazi.
Ukawa wameingia bungeni wote wakiwa
wamevaa mavazi meusi kuashiria kuwa, Bunge
lipo kwenye msiba mzito.
Kwa muda mrefu sasa, wabunge wa upinzani
wamekuwa wakilalamikia Dk. Tulia kuminya
upinzani na kukibeba chama tawala-Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
0 comments :
Post a Comment