Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, June 14, 2016

Wafanyakazi wa sekta ya binafisi na umma nchini kulipwa fidia ya kuumia kazini.soma zaid.

Wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi nchini
wataanza kulipwa fidia ya kuumia kazini kuanzia
Julai Mosi mwaka huu kupitia mfuko wa fidia kwa
wafanyakazi,WCF,ambao umeanzishwa na serikali
kwa mujibu wa sheria.
Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi,WCF,ambao
ulianzishwa na serikali mwaka jana kwa sheria ya
Bunge namba 20 ya mwaka 2008,sasa upo tayari
kuanza kutoa huduma kwa wafanyakazi kuanzia
Julai Mosi mwaka huu,kwa lengo la kukabiliana
na changamoto za wafanyakazi wanaoumia
wakiwa kazini.
Wakati mfuko huo wa fidia kwa wafanyakazi
ukianza kutoa huduma zake,mwakilishi wa
Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo,Dk.Francis
Michael amewaonya waajiri watakaoacha kutoa
au kuchelewesha michango ya wafanyakazi wao
kwamba sheria ya mfuko huo inatoa adhabu kali
ikiwemo faini kubwa na kifugo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya
Mbeya,Katibu Tawala wa wilaya ya
Mbeya,BW.Mbeyela ameutaka mfuko huo
kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya wafanyakazi
watakaojaribu kufanya udanganyifu ili walipwe
fidia kwa lengo la kujinufaisha.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top