Wajasilia mali sasa kuongeza kipato.soma zaid.
Fedha hizo zimetolewa na Hazina Kuu kupitia
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF).
Mkopo huo wenye mrejesho wa asilimia moja kila
mwezi, utahusu vijana hao wanaopewa mafunzo
ya kibiashara na malezi kupitia Taasisi ya
Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TEEC).
Dar es Salaam. Vijana wajasiriamali 3,000
waliopo kwenye makundi mbalimbali katika mikoa
minne nchini watanufaika na mkopo wa Sh500
milioni kwa kipindi cha mwaka wa fedha
2016/17.
Fedha hizo zimetolewa na Hazina Kuu kupitia
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF).
Mkopo huo wenye mrejesho wa asilimia moja kila
mwezi, utahusu vijana hao wanaopewa mafunzo
ya kibiashara na malezi kupitia Taasisi ya
Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TEEC).
Mkurugenzi Mtendaji wa TEEC, Sosthenes
Sambua na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PTF,
Haigath Kitala walisaini makubaliano jana mbele
ya waandishi wa habari tayari kwa uwezeshaji
mitaji wajasiriamali hao wa mikoa ya Dar es
Salaam, Pwani, Lindi na Morogoro.
0 comments :
Post a Comment