Wakuu wa idara 8 wasimamishwa kazi kwa upotevu wa sh.180m kondoa mkoani Dodoma.soma zaid.
Baraza la madiwani la wilaya ya kondoa
limeazimia kusimamishwa kazi kwa wakuu wa
idara wanane kwa upotevu wa shilingi milioni 180
huku wakimuandikia barua waziri wa nchi ofisi ya
rais tawala za mikoa na serikali za mitaa mhe
george simbachawene wakimtaka amrudishe
aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo isdory
mwalongo ili ahojiwe wakimtuhumu kuwa ndio
muusika namba moja wa upotevu huo.
Akisoma maazimio hayo ambayo yalitokana na
Baraza hilo kukaa kama kamati na kujadili
upotevu huo wa pesa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Kondoa Omary Kariati
amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya
madiwani kuridhia wakuu hao wa idara
kusimamishwa huku ikibainika aliyewahi kuwa
Mkurugenzi Bwana. Mwalongo katika upotevu
huo shilingi milioni 34 amesaini hundi yeye
mwenyewe.
Wakizungumza baada ya kufikiwa kwa uamuzi
huo baadhi ya madiwani wamesema wameamua
kuchukua hatua hiyo baada ya kuchoshwa na
vitendo vya ubadhilifu wa fedha katika
halmashauri hiyo ambapo watumishi wake
waliigeuza shamba la bibi huku pia ikinuka
rushwa na dhuluma.
Awali katika baraza hilo mkuu wa wilaya ya
Kondoa Shaaban Kisu amezungumzia
changamoto mbalimbali zinazoikabili wilaya hiyo
ambapo maeneo ambayo yamekuwa na matatizo
kwa muda mrefu ni kwenye migogoro ya ardhi na
uharibifu mkubwa wa Mazingira.chanzo ITV.
0 comments :
Post a Comment