Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, June 5, 2016

Waliotimuliwa UDOM wayiomba serikali kutumia busara zake kuwarudisha chuoni.


Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma
(Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi
waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao
waliambatana na viongozi wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP),
walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa
chuoni.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake,
Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona
wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana
na wao kujiunga na chuo hicho.
Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali
zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni
kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la
kweli.
“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi
wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na
kupata daraja sifuri.
“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango
vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu
na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo
ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na
kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali
itumie busara zake.
“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na
sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”
Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa
Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia
busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo
yao.
Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka
Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili
wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.
“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda
waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni,
kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na
wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa
kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema
Lusako.
Udom yazungumza
Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali
alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri
wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache
daraja la tatu.
“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda
kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa
ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata
ajira ya moja kwa moja,” alisema.
Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa
wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha
wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa
wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango
walichokuwa wamepangiwa.
“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa
ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao
wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa
hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe
nyumbani,” alisema Beatrice.
My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi
mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa
ndani ya masaa 24?
=========================
Tamko la Wanafunzi waliofukuzwa
=========================
Ndugu Waandishi wa habari,
Awali yayote tunapenda kupongeza jitihada
kadha wa kadha ambazo zimekuwa zikifanywa na
serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha
inaboresha mfumo wa Elimu nchini.
Pamoja na ukweli kwamba, kumekuwa na jitihada
mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya
Elimu haswa katika awamu hii ya Uongozi wa
Mh. Raisi, John Pombe Makufuli. Mtandao wa
Wanafunzi Tanzania unasikitishwa na kulaani
baadhi ya maamuzi yaliyokwishafanyika na
kukiuka utu, haki za Wanafunzi na vile vile
taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.
Kuhusu Sakata la Kufukuzwa Wanafunzi UDOM
Mumesikia hoja za viongozi mbalimbali juu ya
sakata la Wanafunzi Waliosimamishwa UDOM,
mmesikia hotuba ya Mh. Joyce Ndelichako,
Waziri mwenye dhamana katika wizara ya Elimu,
lakini vile vile mmesikia hotuba ya Mh. Raisi,
John Pombe Makufuli aliyoitoa akiwa chuo kikuu
cha taifa (UDSM) tar. 02.06.2016
Tangu tar. 28 mei 2016, mara baada ya agizo la
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (MoEST) la
kuwarejesha nyumbani Wanafunzi takribani 7802
Mtandao huu umekua ukifanya tafiti za kina
kupitia idara yake (Reseach& Training
Department) na kupata taarifa za pande zote
mbili kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa
“Wahanga(Wanafunzi waliofukuzwa) na Watawala
(Wizara ya Elimu) ”.
Tumejiridhisha kwamba kitendo kilichofanywa
dhidi ya Wanafunzi wa UDOM ni ukiukwaji
mkubwa wa haki za Wanafunzi ambacho kilikuwa
kwanza cha kimabavu na hakikuzingatia kabisa
utu wa Wanafunzi husika.
Taarifa zilizotufikia ni kwamba Wanafunzi
walifukuzwa kama Wakimbizi ndani ya nchi yao,
Polisi walizagaa kila kona na bunduki zao kama
wanafukuza majambazi, hofu ilitanda na
wanafunzi wengine kuogopa kurudi chuoni kwa
hali ilivyokuwa. Mtandao huu unasikitishwa kwa
matumizi makubwa ya vyombo vya dola lakini
vile vile madhara yaliyowakumba Wanafunzi
husika wakati wa zoezi la kuwaondoa chuoni.
Chimbuko la Mgogoro:
Ikumbukwe, wakati wa uongozi wa Mh. Jakaya
Mrisho Kikwete, kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa Elimu kama vile Mamlaka ya
Elimu (TEA), Tume ya vyuo vikuu (TCU),
Mamlaka ya vyuo vya Ufundi (NACTE) na wadau
mbali mbali a Elimu, waliadhimia na kuzindua
program maalumu ya kusomesha waalimu wa
masomo ya Sayansi katika shule za sekondari
nchini ili kutatua changamoto za uhaba wa
waalimu wa masomo ya sayansi.
Lakini ili kupata waalimu wenye sifa Serikali
ikaweka sifa za Udahili kwamba itakuwa kwa
wahitimu wa kidato cha nne tu waliopata daraja
la 1,2 na 3 pia wawe na ufaulu wa alama A” au
B” kutoka masomo ya sayansi. Na serikali
ikawashawishi kwa ahadi ya kuwapa mkopo kwa
100%.
Tumeshangazwa kwamba, Sababu za
kusimamishwa masomo wanafunzi hawa
zimeendelea kubadilika badilika, sababu ya
kwanza kabisa, ambayo ilisemwa na Prof. Joyce
Ndelichako Bungeni ni Mgomo wa Wahadhiri
uliotokana na kukosa posho za kuwafundisha
Wanafunzi husika, Sababu ya pili ni wanafunzi
kukosa sifa.
Mtandao huu umejiuliza, Kama suala kuu ni
vigezo kwanini serikali isingeweka utaratibu
maalumu wa kuwaondoa wanafunzi wasio na sifa
na kuwawajibisha wale waliowadahili kinyume na
standard zilizowekwa na serikali?
1. Tunapenda Kutumia fursA hii kukanusha
taarifa zote za uongo zilizotolewa na watawala/
Viongozi dhidi ya wanafunzi husika. Na
kumekuwa na utamaduni wa Watawala kutumia
Vyombo vya habari(Media coverage) kama silaha
ya kupotosha taarifa kwa umma(Taarifa hii
itasomwa na muwakilishi wa wahanga wa
Wanafunzi (UDOM)
Ombi letu.
1. Tunaiomba serikali kupitia wizara yake ya
Elimu ifanye hima kuwarudisha Wanafunzi husika
ili kutoendelea kupoteza rasilimali muda wa
wanafunzi husika
2. Kama hotuba ya Mh. Raisi hapo juzi katika
chuo kikuu cha Dar es Salaam, akikiri kwamba
kunawanafunzi wasio na vigezo walidahiliwa.
Mtandao huu unaomba waliohusika kuwadahili
wawajibishwe haraka iwezeanavyo lakini vile vile
wanafunzi wafidiwe Rasilimali fedha na muda
waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni.
Hatma ya Wanafunzi (UDOM)
Kama itatokea, kunamwanafunzi au kundi Fulani
la Wanafunzi, halitopewa haki zake, Mtandao huu
utashirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu
zikiwemo azaki zinazojihusisha na masuala ya
utetezi kisheria kutafuta haki za Wanafunzi
husika mahakamani
Chanzo cha Migogoro katika Sekta ya Elimu
Nchini.
v Kutokuwa na Muafaka wa Kitaifa katika Mfumo
wa Elimu.
Mtandao huu unaamini kwamba haya yote ni
madhara ya kutokuwa na muafaka wa kitaifa/
Msimamo wa itaifa katia Sekta ya Elimu nchini.
Kwa mda mrefu, mfumo wetu wa Elimu, Sekta ya
Elimu nchini imekuwa inaendeshwa na kiwango
cha utashi wa Waziri wa Elimu aliyepo
madarakani na sio kuongozwa na dira/Muafaka/
Msimamo wa kitaifa katika sekta ya Elimu.
Tumeshuhudia, Mawaziri wa Elimu tofauti tofauti,
katika awamu tofauti tofauti za uongozi tangu
uhuru wa nchi hii (Mh.Jumanne Maghembe, Mh,
Joseph Mongai, Mh. Shukuru Kawambwa na sasa
Mh. Joyce Ndalichako), wakifanya maamuzi
kutokana na kiwango cha utashi wao na mapenzi
yao. Hii ni hatari katika taifa letu na
imesababishwa na ukweli kwamba taifa limekosa
dira/Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu
nchini.
Hitimisho.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania unaamini
kwamba kilichotokea Chuo Kikuu cha DODOMA
kitakuwa msingi wa Serikali kupitia Wizara ya
Elimu kuanza harakati rasmi za kimapinduzi za
kuunganisha wadau wote wa Elimu nchini ili
kuwa na mjadala mpana wa kitaifa wa namna ya
kufikia Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu
nchini.
Vile vile Mtandao huu umeshaandaa waraka
maalumu kwa Waziri wa Elimu unaotoa
muongozo wa namna taifa litakavyofanikisha
kuwa na Muafaka wa kitaifa katika sekta ya
Elimu nchini ambao tutauwasilisha wizarani
mapema wiki ijayo.
Mwisho kabisa, tunaomba viongozi wote wa dini
na wale wanaoamini, kuendelea kumwombea Mh.
Raisi n a viongozi wengine ili waongoze taifa hili
kwa hekima na busara na kwa kufuata taratibu,
kanuni na sheria za nchi hii

0 comments :

Post a Comment

Back To Top