Aliyekuwa mkugurugenzi halimashauri ya Hanangi matatani.soma zaid.
Hanang. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dk Joel
Bendera ameagiza aliyekuwa Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hanang’
Filex Mabula na Aliyekuwa mweka hazina wa
Halmashauri hiyo Matonya Mizengo wafikishwe
mahakamani kujibu mashitaka ya upotevu wa
Sh932 milioni.
Akizungumza juzi wilayani Hanang Dk Bendera
alisema taarifa ya uchunguzi wa tuhuma za
ubadhirifu wa fedha zilizokuwa zinawakabili
Mabula na Mizengo waliosimamishwa tangu Aprili
6 mwaka huu, zimewaingiza hatiani.
Dk Bendera alisema kamati hiyo ilibaini kuwa
Mabula na Matonya wameisababishia
halmashauri hiyo madeni ikiwamo hospitali ya
wilaya (Tumaini) inayodaiwa na Bohari ya Dawa
(MSD) Sh34.606 milioni hivyo wamepoteza sifa
za utumishi na wafikishwe mahakamani.
0 comments :
Post a Comment