Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, June 5, 2016

Kifo cha Ali kimefanya wagombea urais marekani kushutumiana kwa maneno makali..soma zaid.

Kifo cha Muhammed Ali kimezua malumbano
makali katika ulingo wa kisiasa miongoni mwa
wagombea wa kiti cha Urais katika uchaguzi
mkuu, utakaofanyika mwezi Novemba nchini
Marekani.
Katika risala zake za rambirambi mgombea wa
kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha
Republican, Donald Trump, amesema kuwa Ali
kwa hakika alikuwa Bingwa ambaye
atakumbukwa na wengi.
Mwaka Jana, Ali alilaani wito uliotolewa na
Bwana Trump, ya kuwazuia kabisa waislamu
kuingia nchini Marekani.
Kwa upande wake mgombea wa kiti cha Urais
kwa tiketi ya chama cha Democratic, Seneta
Bernie Sanders, amemshutumu Bwana Trump na
kumtaja kuwa mnafiki.
Naye Bi Hillary Clinton, amesema kuwa Bwana
Trump, anafaa kuhukumiwa kwa matamshi yake
anayotoa.
Bondia huyo alifariki siku ya Ijumaa huko Arizona,
na alikuwa akiugua maradhi ya kusahau- sahau,
kwa zaidi ya miaka thelathini.chanzo BBC Swahili.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top