Rais apokea ripoti juu ajira ya watoto wa vigogo wanaofanya kazi (BIOT).soma zaid.
Hatimaye ile ripoti iliyokuwa inasubiriwa kwa
hamu inayotishia hatima ya ajira za watoto
kadhaa wa vigogo ndani ya Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), imekamilika na kuwasilishwa
mezani kwa Rais John Magufuli, Ikulu.
Inasemekana kwa sasa hali si shwari BoT, baad
ya kuwepo tetesi za kupunguza watumishi
ambao wengi ni watoto wa vigogo waliongia kw
migongo ya wazazi wao.
Akizungumza na Nipashe jana, Gavana wa BoT,
Prof. Benno Ndulu, alisema maagizo ya Rais
Magufuli juu ya kupitia upya ajira za watumishi
wote wa taasisi hiyo yameshafanyiwa kazi na
ripoti yake imekamilika.
Machi 10 mwaka huu, Rais Magufuli alifanya
ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya BoT na
kutoa maelekezo mbalimbali kwa menejimenti y
taasisi hiyo nyeti kwa mustakabali wa taifa
kiuchumi.
Rais Magufuli alimuagiza Gavana wa BoT (Prof.
Ndulu) kupitia upya ajira za watumishi wa taasis
hiyo na kupunguza idadi ya watumishi hao hasa
ikibainika kuwa kazi zao zinaweza kufanywa na
watu wengine.
Katika mazungumzo yake hayo na uongozi wa
BoT, ilibainika kuwa benki hiyo ina watumishi
takriban 1,391; idadi ambayo ilionekana kuwa ni
ya juu kulinganisha na ukubwa wa taasisi hiyo n
hivyo kumshangaza Rais Magufuli.
Wakati akizungumza na Nipashe jana, Prof. Ndul
alisema kazi hiyo (ya kupitia ajira za watumishi)
ilishafanyika na ripoti yake imeshawasilishwa
kwenye vyombo husika.
"Hiyo kazi ilishafanyika kama alivyoagiza
Mheshimiwa Rais na tayari vyombo vinavyohusik
vimeshapewa taarifa hiyo," alisema Prof. Ndulu
na kuongeza:
"Hatutoi taarifa kama hizo magazetini bali
kwenye vyombo husika--sisi tukishakamilisha ka
tunapeleka ripoti kwenye mamlaka husika na
ndivyo tulivyofanya."
AJIRA ZA WATOTO WA VIGOGO
Alipotembelea benki hiyo Machi, Rais Magufuli
alisema anashangazwa kuwapo kwa wafanyakaz
wengi ndani ya BoT ambao baadhi hata kazi
wanazofanya hazijulikani wazi.
"Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la
wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata
kazi wanazofanya hazijulikani," alinukuliwa Rais
Magufuli.
Kabla ya ziara ya Rais Magufuli, majina kadhaa
ya watumishi wa BoT yalikuwa yakiibua mijadala
mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kwa
madai kuwa ajira zao zimetokana na kubebwa n
wazazi ama ndugu zao ambao wana ushawishi
mkubwa serikalini kutokana na nafasi mbalimbali
walizo nazo au kuwahi kuwa nazo.
Orodha ya watu wanaodaiwa kuwa ni ya watoto
wa vigogo, na ambayo Prof. Ndulu alisema siyo
mpya kwani ilishaandikwa na kujadiliwa sana
hapo kabla ni pamoja na Pamela Lowasa,
anayedaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri
Mkuu, Edward Lowasa.
Wegine ni Filbert Sumaye anayedaiwa kuwa ni
mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu katika serikali ya
awamu ya tatu, Fredrick Sumaye na Zaria
Kawawa, anayedaiwa ni mtoto wa aliyewahi
kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya
kwanza, Marehemu Rashid Mfaume Kawawa.
Mwingine ni Harriet Lumbanga anayedaiwa ni
mtoto wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi
wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tatu
Marten Lumbanga.
Aidha, orodha hiyo pia ina jina la Salama Ali
Hassan Mwinyi anayedaiwa ni mtoto wa
aliyekuwa Rais wa awamu ya pili, Alhaji Hassan
Mwinyi; Rachel Muganda anayedaiwa ni mtoto
wa aliyekuwa Balozi katika serikali ya awamu ya
nne, Alexender Muganda. Salma Omar Mahita,
katika orodha hiyo anadaiwa kuwa ni mtoto wa
aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wakati wa
utawala wa awamu ya tatu, IGP mstaafu Omar
Mahita.
Wengine ni Justina Joseph Mungai anayedaiwa
kuwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri wa
Elimu na Utamaduni katika serikali ya awamu ya
tatu, Joseph Mungai. Pia yumo Keneth Nchimbi
anayehusishwa na kada wa CCM aliyewahi kuwa
kigogo wa Jeshi la Polisi John Nchimbi. Blasia
William Mkapa, anadaiwa kuwa ni mtoto wa Rais
wa awamu ya tatu, Benjamin Mkpa katika orodh
hiyo yenye pia jina la Violet Phillemon Luhanjo,
ambaye anadaiwa kuwa mtoto wa aliyewahi
kuwa Katibu Mkuu kiongozi wakati wa serikali y
awamu ya tatu na nne, Phillemon Luhanjo.
Liku Kamba anadaiwa kuwa mtoto wa aliyekuwa
kada wa CCM wa muda mrefu, Kate Kamba.
Wengine wanaotajwa katika orodha hiyo ni
Thomas Mongela anayedaiwa kuwa mtoto wa
kada mashuhuri ndani ya CCM; aliyewahi kushik
nyadhifa mbalimbali zikiwamo za ubunge,
Getrude Mongela. Jina la Jabir Abdalah Kigoda
linadaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri w
Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu y
nne, marehemu Abdalah Kigoda.
Machi mwaka huu, mara baada ya agizo la Rais
Magufuli kuhusiana na ajira za watumishi wa
taasisi hiyo, Nipashe ilizungumza na Prof.
Ndulu kwa njia ya simu kutaka kujua kama kweli
orodha ya watoto hao ni miongoni mwa
watumishi wa BOT na majibu yake kwa
mwandishi, ambaye alimsomea majina hayo
kuanzia mwanzo hadi mwisho, ni kwamba orodh
hiyo 'haina jipya'. Prof.
Ndulu alieleza zaidi kuwa hakuna ubaya wowote
kwa mtu mwenye sifa kuajiriwa na BoT, bila kuja
jina lake.
"Hayo majina kwani kwako wewe ni mapya?
Mbona yameshaandikwa na kujadiliwa sana
hayo--mimi nasema hakuna jipya hapo," alisema
Profesa Ndulu na kuongeza:
"Hivi ukiwa na jina kubwa halafu ukiwa na akili
ama sifa za kufanya kazi fulani, unataka
kuniambia usipewe hiyo kazi kwa sababu una jin
kubwa?"
HOFU YATANDA
Licha ya ufafanuzi wa Prof. Ndulu kuhusiana na
madai ya kuwapo kwa watumishi walioajiriwa
kwa sababu ya ushawishi wa wazazi wao amba
ni vigogo serikali, bado mijadala mbalimbali
iliendelea kutawala katika mitandao ya kijamii
kuhusiana na orodha hiyo.
Aidha, imedaiwa kuwa hofu imetanda miongoni
mwa watumishi hao na wengine wengi kutokana
na kile kinachoelezwa kuwa huenda kukawa na
punguzo kubwa la watumishi kutoka idadi iliyopo
sasa ya wafanyakazi 1,391; jambo ambalo
linaweza kutekelezwa wakati wowote kulingana
na kile kilichomo ndani ya ripoti na kumfikia Rai
Magufuli.
Wengi wa wachangiaji katika mitandao ya kijami
kuhusiana na majina ya watoto wa vigogo ni
madai kwamba ajira zao zilitokana na ushawishi
wa majina makubwa ya wazazi wao katika
medani za uongozi nchini na siyo sifa za
kuajiriwa kwenye taasisi hiyo na hivyo, upo
uwezekano kuwa wengi miongoni mwao
hawatasalimika pindi kazi ya kuwapunguza
watumishi (wa BoT).
Source: Nipashe
0 comments :
Post a Comment