Wanachuo st.joseph kampasi ya Dar es salaam wameipeleka TCU mahakamani.soma zaid.
Nadhani sote tunakumbuka Wanafunzi
316 waliosimamishwa masomo chuo
kikuu cha St. Joseph Kampasi ya Dar es
salaam, walifungua kesi ya kuomba kibali
cha kuwakilisha wenzao mahakamani
pamoja na chuo kusitisha masomo wakati
kesi ya msingi ikiendelea kusikilizwa.
Sasa kesi hiyo imetajwa leo June 10 2016
Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam
ambapo imetoa kibali kwa wanafunzi
kufungua kesi dhidi ya chuo hicho na
Tume ya vyuo vikuu Tanzania ‘TCU’.
Leo hii akitoa ufafanuzi wakili wa
walalamikaji, Emmanuel Muga amesema
amenukuliwa akisema ’hii kesi ina
utaratibu kwa sababu mpo wengi
wanafunzi 316 ikiwa ni watu wengi inabidi
upande kibali cha mahakama ili ufungue
hiyo kesi na hiyo kesi itawakilishwa na
watu wachache yaani watu wanne tu
lakini ili watu wanne wawakilishe wenzo
wote lazima mahakama itoe kibali’
Katika madai ya msingi, walalamikaji
ambao ni wanafunzi wanadai fidia ya
miaka mitatu waliokaa chuoni hapo dhidi
ya chuo na Tume ya vyuo vikuu Tanzania
‘TCU’.
0 comments :
Post a Comment