Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, June 11, 2016

Maadhimisho ya siku ya utumishi wa umma yafutwa.soma zaid.

Waziri wa Utumishi wa Utawala Bora, Angellah
Kairuki
Serikali ya Tanzania imebadilisha mfumo wa
maadhimisho ya siku ya utumishi wa umma
badala yake siku hiyo ya tarehe 16 hadi 23
mwezi huu itatumika kwa watendaji wakuu wa
wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na taasisi
za serikali kusikiliza kero za watumishi wa umma
katika maeneo yao ya kazi kwa lengo la
kuzitafutia ufumbuzi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na
Utawala Bora Mh. Angellah Kairuki amesema
hakutakuwa na maonesho katika viwanja vya
Mnazi Mmoja kama ilivyozoeleka kwani bado
kuna changamoto nyingi zinazowakabili
wafanyakazi na hivyo vyema siku hiyo
wakasilizwa ili kutatuliwa.
Aidha katika hatua nyingine waziri Kairuki
amesema kuanzia tarehe 1 Machi mwaka huu
hadi tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu jumla ya
watumishi 12,246 wameondolewa kwenye mfumo
wa malipo ya miashahara kwa sababu mbalimbali
zikiwemo za kutimiza umri wa kustaafu kwa
lazima, kufariki au kufukuzwa kazi.
Amesema katika zoezi hilo pia jumla ya shilingi
25,091,292,688,82 zingepotea kama watumishi
wasingeondolewa kwenye mfumo ikilinganishwa
watumishi 10,295 walioondolewa kwenye mfumo
hadi tarehe 30 Aprili mwaka huu na jumla ya
shilingi 23,206,547,598.82 zilizookolewa ambapo
hilo ni ongezeko la watumishi 1,951 na shilingi
1,884,745,090.chanzo eat Africa television

0 comments :

Post a Comment

Back To Top