Warepublikan na wademokrat wamemshutumu Donard Trump kwa matamshi yake.soma zaid.
Katika hali ya nadra ya umoja katika kipindi cha
uchaguzi imejitokea baada ya Warepublikan na
Wademokrat kumshutumu anayetazamiwa kuwa
mgombea urais wa chama cha Republican
Donald Trump kwa matamshi yake kuhusu asili
ya jaji anayesimamia kesi ya chuo kikuu
inayomkabili Bwana Trump.
Wanachama wa vyama vyote walipinga kauli ya
bilionea huyo na kuiona kuwa ni ya ubaguzi wa
rangi.
Bwana Trump alisema kwamba jaji wa
mahakama ya mwanzo ya Marekani, Gonzalo
Curiel, hatoweza kusimamia kesi yake kwa haki
kwa sababu ya asili yake ya Mexico. Jaji huyo ni
Mmarekani aliyezaliwa na kukulia katika jimbo la
Indiana, hapa Marekani.
0 comments :
Post a Comment