Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, July 14, 2016

Al shabaab yahofiwa kuhusika na mauaji ya polisi nchini kenya.soma zaid

Maafisa wanne wa polisi wanahofiwa kufariki
baada ya mtu mshukiwa wa ugaidi kumpokonya
askari bunduki na kuwafyatulia maafisa wa
Polisi.
Yamkini mshukiwa huyo wa ugaidi alikuwa
amefungiwa korokoroni baada ya kukamatwa kwa
tuhuma za kujaribu kuwashawishi watu kujiunga
na mtandao wa kigaidi wa Al Shabaab.
Alipelekwa katika kituo cha polisi cha
Kapenguria, Kaskazini Magharibi mwa Kenya.
Awali gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa mtu
huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho kumnusuru
mshukiwa aliyekuwa amekamatwa kwa tuhuma
za ugaidi .
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano
wameuawa.
Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido
anadaiwa kujeruhiwa.
Ufyatulianaji wa risasi bado unaendelea.
Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu mkuu
wa polisi Joseph Boinnet akisema polisi zaidi
wametumwa eneo hilo.
“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa
alitwaa bunduki na kuanza kuvyatua risasi," Bw
Boinnet amenukuliwa. "Kituo hicho sasa
kimezingirwa na juhudi za kukabiliana naye
(mshambuliaji) zinaendelea."

0 comments :

Post a Comment

Back To Top