Hii ni taarifa kutoka NACTE kuhusu mfumo wa udahili wa pamoja.soma zaid.
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS)
umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai
2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi
baada ya Baraza kuchagua waombaji
udahili waliowasilisha maombi yao
kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3
Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi
ni tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.
Waombaji wapya na baadhi ya waombaji
walioshindwa kukamilisha maombi yao
kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni
2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha
maombi ya udahili kupitia Mfumo wa
Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi
zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa
kutumia muda huu wa nyongeza ili
kuwasilisha maombi.
Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji
udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao
vya Kamati za kuidhinisha majina ya
waombaji udahili kupitia Mfumo wa
Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha
orodha ya majina ya wenye sifa za udahili
kulingana na nafasi za udahili kwa kila
kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya
tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai 2016.
Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa
kila kozi itolewayo na chuo husika
yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa
Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji
waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia
kurasa (profile) zao binafsi au
kwa kubofya hapa.
Waombaji ambao hawakuchaguliwa
wamejulishwa sababu zilizowafanya
wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao
pia.
Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza
waliowasilisha maombi yao kupitia
NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu
kuwa, mashauriano kati ya NACTE na
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
yanaendelea kufanyika ili kufanikisha
udahili wa waombaji wa kozi za Shahada
ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
0 comments :
Post a Comment