Kanisa la KKKT lasalimu amri lipo layari kurudisha sh.29 ml.soma zaid.
Arusha. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) la Mjini Kati, Dayosisi ya Kaskazini
mkoani Arusha, limesema lipo tayari kurudisha
Sh129 milioni ambazo zilitolewa na Serikali kwa
ajili ya mishahara ya madaktari katika Hospitali
ya Selian ambayo linaimiliki.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuwahoji
baadhi ya watumishi wa kanisa hilo na
kuchukua baadhi ya mafaili kwa kile
kilichoelezwa kwamba wanachunguza
mishahara hewa.
Katibu wa Dayosisi hiyo, Samwel Saiguran
alisema juzi ofisini kwake kwamba wapo tayari
kurudisha kiwango hicho cha fedha kwa
utaratibu, kwani waliwalipa madaktari ambao
hawakuwa katika orodha ya watumishi wa
Serikali kwa nia njema kuokoa maisha ya
Watanzania.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha,
Juventus Baitu alisema taasisi yake inafanya
uchunguzi kuhakiki watumishi hewa Hospitali ya
Selian inayomikiliwa na kanisa hilo lakini
hakutaka kuingia undani wa suala hilo.
0 comments :
Post a Comment