Jeshi la Polisi nchini limekamata vipande vya meno ya tembo 666.soma zaid.
JESHI la Polisi nchini kwa kishirikiana na Ofisi za
Interpol Kanda ya Kusini Mwa Afrika imefanya
operesheni na kukamata vipande vya meno ya
Tembo 666 vyenye uzito wa Kilogram 1279.19
vyenye thamani zaidi ya a Sh. Biloni Nne.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Jeshi la Polisi
(CP), Diwani Athuman wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
amesema kuwa vipande hivyo vya tembo
yamehusisha watu tisa kati yao mmoja ni Raia
wa Guinea na mwingine ni Raia wa Uganda.
Amesema kuwa katika operesheni Usalama III
wameweza kukamata vitu mbalimbali kutokana
na taarifa za kiitelijensia zilizokusanywa wakati
wa matayarisho ya operesheni ya Usalama III,
ambapo waliweza kukamata mitambo ya 18 ya
kutengenezea gongo pamoja na lita za gongo
960 zimekamatwa.
0 comments :
Post a Comment