Mkoa wa katavi unaongoza kwa watoto wa kike wenye umri mdogo kuwa na mimba.soma zaid.
Dar es Salaam. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
imesema mkoa wa Katavi ndio unaoongoza kwa
kuwa na idadi kubwa ya wasichana wanaopata
mimba wakiwa na umri mdogo.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya
idadi ya watu duniani, Mkurugenzi wa NBS Albina
Chuwa alisema takwimu zinaonyesha mkoa huo
unaongoza kwa asilimia 36.8, Tabora 36.5 na
Simiyu 32.1 huku Dar es Salaam ukiwa mwishoni
kwa asilimia 12.
kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la watu
duniani (UNFPA), Tanzania ni miongoni mwa nchi
tatu zinazoongoza kwa tatizo hilo barani Afrika.
Kutokana na hali hiyo, Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Ummy
Mwalimu aliitaja jamii kutoendeleza vitendo vya
udhalilishaji kwa watoto wa kike, huku akidai
kuwa lazima hatua za haraka za kukabiliana na
tatizo hilo zifanywe.
Awali Mkurugenzi wa huduma za afya wa Shirika
la Maria Stopes, Dk Joseph Komwihangiro
alisema ili kupambana na hali hiyo lazima
wasichana wapewe elimu kuhusu masuala ya
uzazi ili waweze kujilinda na ndoa za utotoni.
Takwimu zinaonyesha zaidi ya asilimia 10 ya
wasichana walio na umri mdogo wameanza
kutumia njia za uzazi wa mpango.chanzo mwananch
0 comments :
Post a Comment