Madereva wa Bodaboda watoa mchango wa katika ujenzi wa wodi mbeya.soma zaid.
Madereva hao kupitia chama chao kijulikanacho
kama Umoja wa Waendesha Bodaboda na
Wamiliki Bodaboda Mbeya (Uwabomu), wametoa
mifuko 75 ya saruji yenye thamani ya Sh milioni
1.03 ikiwa ni mchango wao katika ujenzi wa wodi
ya watoto unaoendelea katika Hospitali ya Rufaa
Kanda ya Mbeya.
Mifuko hiyo ilikabidihiwa kwa uongozi wa
hospitali hiyo ya rufaa na Mwenyekiti wa
Uwabomu, Asajile Lisyele katika hafla fupi,
iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Sisi na
bila shaka Watanzania wengine, tungependa
kuwapongeza kwa dhati wanachama wa
Uwabomu kwa kitendo hicho cha kuisaidia jamii
yetu yenye mahitaji muhimu, kama ya wodi kwa
ajili ya watoto wetu.
Uamuzi wa kujitolea kuchangia huduma za jamii
tena kutoka kwa wananchi, wanaoendesha
maisha yao kupitia biashara ya bodaboda ni
mfano wa kuigwa siyo tu na wanabodaboda
wengine nchi nzima, bali pia wajasirimali
wengine.
Kwa hali hii ya kujitoa kwa bodaboda hao, ni
ushahdi tosha kwamba kumbe huhitaji kuwa tajiri
ili kuweza kuchangia huduma za jamii kama
ujenzi wa wodi, bali utu na moyo wa kujitoa kwa
ajili ya kujali wengine katika jamii.
Lakini pia huo ni mwanzo na mfano mzuri kwa
wenzetu, wanaoendesha biashara ya bodaboda
kuanza kurejesha imani kwa wananchi na serikali
kutokana na mtazamo, hasa kwamba kufanya
biashara ya bodaboda ni virugu, watu wasiotaka
kufuata sheria na taratibu za biashara ya
uendeshaji wa vyombo vya moto kutokana na
vitendo viovu, vinavoshuhudiwa katika maisha ya
kila siku ya biashara hiyo kwa watendaji wake.
Kama Uwabomu wameweza kujitolea kuchangia
katika utaratibu mzuri kiasi hiki, tunapenda
wanabodaboda nchini kote, waige mfano wa
wenzao wa Mbeya, siyo kwa kujitoa kuchangia
jamii kwa masuala ya maendeleo mbalimbali, bali
pia kubadilika katika utendaji wao wa kila siku
wa biashara yao ya bodaboda ili jamii waone
mabadiliko yao kwa vitendo na ustaarabu
unaostahiki.
Hakuna ubishi kwamba wanajamii wengi
wanaowaona bodaboda kama ni kero kutokana na
ukweli kwamba wengi wao hawafuati sheria za
barabarani, hufanyakazi zao huku wakiwa na
viroba; au tayari wamelewa kinywaji kingine na
pia hawaishi kugombana na watumiaji wengine
wa barabara, wakiwemo wenye magari na
waenda kwa miguu.
Wakati umefika sasa kuchukua hatua za
makusudi, kubadilisha hali hiyo ili sote tunufaike
vilivyo kwa huduma, kipato na ustawi wetu.
Huduma hii tunaihitaji na kwa kweli inatoa ajira
kwa vijana wetu wengi, lakini taabu yake ni
kutozingatia sheria na taratibu. Tubadilike na
hongera sana Uwabomu kwa kuwa mfano wa
kuigwa na wengine.chanzo habar leo
0 comments :
Post a Comment