Wanafunzi wa vyuo vikuu 2 Dar wafikishwa mahakani kwa mauaji.soma zaid
WATU watatu wakiwemo wanafunzi wawili wa
vyuo vikuu vilivyoko jijini Dar es Salaam
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
wakikabiliwa na mashitaka ya mauaji.
Wanafunzi hao ni wa Chuo Kikuu cha Ardhi,
Hussein Mustafa (26) na wa Chuo Kikuu Huria
(OUT), Haruna Nkuye (24) ambao
wanashitakiwa pamoja na fundi makenika
Rajabu Ally (41) wote wakazi wa Dar es
Salaam.
Washitakiwa hao wanaodaiwa kuhusika na
mauaji hayo kwenye tukio la ujambazi katika
Benki ya CRDB eneo la Chanika Wilaya ya Ilala,
Dar es Salaam, walisomewa mashitaka na
Wakili wa Serikali Jackson Chidunda mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi.
Akisoma hati ya mashitaka, Chidunda alidai
Desemba 8, mwaka jana katika eneo la Chanika,
Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, washitakiwa
walimuua Ramadhani Halili, Shan Rajabu na
Thomas Otemu.
Hakimu Shahidi alisema washitakiwa
hawatakiwi kujibu mashitaka kwa kuwa
mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza
shauri hilo isipokuwa Mahakama Kuu.
Upande wa jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa
kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe
nyingine ya kutajwa ili wamuunganishe
mshtakiwa Mohamed Ungando ambaye jana
hakuwepo mahakamani.
Awali, mshitakiwa Mustafa aliiomba mahakama
imsaidie apate matibabu kwa kuwa viungo
vinamuuma kutokana na adhabu alizopewa
akiwa mahabusu.
Hakimu Shahidi alisema gerezani kuna utaratibu
wa matibabu, kama hatatibiwa kesi itakapotajwa
tena aijulishe mahakama. Kesi hiyo
imeahirishwa hadi Julai 14, mwaka huu.chanzo mpekuzi blog
0 comments :
Post a Comment