Breaking News
Loading...

Advert

Monday, July 11, 2016

Jeshi la polisi hapa nchini linafanya uchunguzi dhidi ya hili.soma zaid

JESHI la Polisi nchini, limesema linafanya
uchunguzi kubaini baadhi ya vijana wanaojiunga
na vikundi vya kigaidi, vikiwamo IS na Al-
Shabaab ili wawachukulie hatua za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, alisema
wimbi la vijana hao kujiunga na makundi hayo
yanayopigwa vita duniani kote, linatokana na
ushawishi wa baadhi ya watu.
“Tuna taarifa za kuwapo baadhi ya vijana wa
Kitanzania wanaojiunga na vikundi vya ugaidi…
suala hili ni la kiintelijensia zaidi, hatuwezi
kulizungumzia kiundani, tunaendelea kulifanyia
kazi, tutakapofikia sehemu nzuri tutawaambia,”
alisema Athuman.
Alisema wakati suala hilo linaendelea kufanyiwa
kazi, jeshi hilo liliendesha operesheni maalumu
ya siku mbili, ambayo ilishirikisha nchi 26 za
Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Alizitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda, Burundi, Angola, Botswana,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
Lesotho, Malawi, Madagascar, Mauritius,
Msumbuji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland,
Zambia, Zimbabwe, Comoro, Djibouti, Eritrea,
Ethiopia, Shelisheli, Sudan Kusini na Somalia.
Alisema operesheni hiyo iliyojulikana kama
‘Operesheni Usalama III’ ilishirikisha nchi zaidi
ya 26 na ilisaidia kukaguliwa kwa magari 1,632
ambayo kati ya hayo, 10 yalikuwa ya wizi huku
matano yalibainika yameingiliwa ‘chases’.
Alisema operesheni hiyo pia ilisaidia
kukamatwa pikipiki 12 za wizi, huku 18
zikiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana
na kutokuwa na vibali halali.
Athuman alisema operesheni hiyo ilisaidia pia
kukamatwa aina mbalimbali ya dawa za
kulevya, zikiwamo heroine gramu 83, bangi
kilogramu 398.6, mirungi kilogramu 30, bunduki
aina ya shotgun moja, gobole 11, risasi 104,
mkuki mmoja na vipande 15 aina ya exprojel v6,
cotex na detonator.
Alisema walikamata wahamiaji haramu 43
maeneo mbalimbali nchini, kati yao 18 ni raia
wa DRC, ambao walikamatwa mikoa ya Rukwa
na Kagera, wakati 22 wanatoka Burundi
waliokamatwa mikoa ya Shinyanga, Tabora na
Kagera na raia wawili wa Rwanda walikamatwa
Kagera na mmoja wa Kenya alikamatwa Tabora.
“Katika operesheni hii tulifanya ukaguzi katika
kampuni mbalimbali zinazofanya biashara ya
madini ambapo tatu zilionekana kukosa uhalali wa
kupewa leseni ya kuendelea kufanya biashara ya
madini,
“Kampuni hizi ni Delicore Metal Company Ltd,
Madandwa Gold Mining Export Import (T) Ltd na
Alex Mining Co. Ltd, na tatizo lao linaendelea
kushughulikiwa na Wizara ya Nishati na Madini.
Pia yalikamatwa madini aina ya Acquqmiline
Smoky Quartz kilogramu 20.
Alisema pia walikamata gamba moja la kasa
mkoani Ruvuma, mbao 410 zilizokuwa
zikisafirishwa bila kibali mikoa ya Pwani, Iringa
na Morogoro, nyama ya pundamilia kilo 45 na
bidhaa bandia.chanzo mpekuzi blog

0 comments :

Post a Comment

Back To Top