Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, July 12, 2016

Mahakama kuu nchini uganda imempa dhamana Kizza Besigye.soma zaid.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza
Besigye, ambaye amezuiliwa kwa wiki kadha,
amepewa dhamana na Mahakama Kuu nchini
humo.
Jaji Wilson Masalu Musene amempa kiongozi
huyo wa chama cha Forum for Democratic
Change dhamana ya dola 30,000 za Marekani.
Jaji amemwamuru Dkt Besigye kutojihusisha na
vitendo vya kuzua ghasia na adumishe amani
katika jamii hadi kesi ya uhaini inayomkabili
isikizwe na uamuzi kutolewa.
Mwana wa Besigye ashinda urais Oxford
Ametakiwa awe akifika kortini mara moja kila
wiki mbili kuanzia Julai 26.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, wafuasi
wa Beisgye wameimba wimbo wa taifa wa
Uganda na kushangilia baada ya kiongozi wao
kupewa dhamana.
Besigye amerejeshwa seli kusubiri kukamilishwa
kwa utaratibu wa kumwachilia huru kwa dhamana
hiyo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top