Breaking News
Loading...

Advert

Monday, July 11, 2016

Mvutano unaendelea kati ya korea Kaskazini na Marekani.soma zaid.

Maafisa wa runinga inayothibitiwa na serikali ya
Korea Kaskazini, wanasema kuwa serikali ya
nchi hiyo itakata mawasiliano na Marekani.
Korea Kaskazini inasema kuwa utawala wa
Washington tayari umefahamishwa sababu ya
hatua hiyo.
Aidha Korea imesema kuwa maswala ambayo
bado yanajadiliwa ikiwa ni pamoja na kukamatwa
kwa wamarekani wawili sasa yatajadiliwa chini
ya sheria kali za kivita.
Korea Kaskazini inasema hatua hiyo imeafikiwa
katika kile kinachotajwa kama sheria ya kivita.
Shirika hilo la sereikali aidha linasema kuwa
imeafikia hatua hiyo baada ya Marekani
kumuorodhesha rais wa nchi hiyo Kim Jong-un
katika orodha ya wale waliopigwa marufuku
kutokana na rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki
za kibinadamu.
Wakati huohuo Korea Kaskazini imeapa
kudungua manuari yeyote ya kivita itakayolenga
roketi zake za masafa marefu.
Marekani na Korea Kusini zimetangaza mipango
ya kuweka Mfumo wa ulinzi wa Terminal High
Altitude Area Defense (THAAD) unaolenga
kudungua makombora ya masafa marefu ya
Korea kaskazini.
Korea kaskazini imeonya kuwa hilo ni dhihirisho
la mataifa hayo kuichokoza na hivyo kutangaza
vita dhidi yao .
Hata hivyo haijajulikana Marekani na Korea
Kaskazini zitaiweka wapi mtambo huo wa ulinzi
wa kisasa na yupi kati ya washirika hao wawili
watauendesha mtambo huo wenye uwezo
mkubwa wa ulinzi dhidi ya Makombora.chanzo bbc

0 comments :

Post a Comment

Back To Top